Halmashauri ya manispaa ya Bukoba mkoani Kagera imeanza kuchukua tahadhari dhidi ya mafuriko yanayoweza kuikumba manispaa hiyo kwa kusafisha na kuzibua mitaro ya maji pamoja na kuimarisha usafi wa mazingira kuanzia ngazi ya familia.
Zoezi hilo likuja siku chache baada ya mamlaka ya hali ya hewa kutoa tahadhari ya maeneo zaidi nchini kukumbwa na mafuriko, ambapo linafanyika kila siku ya alhamisi na linasimamiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe ambaye alionya kuwa mwananchi yeyeto atakayekaidi kutekeleza zoezi la usafi kwenye eneo lake atalazimika kulipia faini ya kati ya shilingi elfu ishirini hadi hamsini ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaoshindwa kudumisha usafi kwenye maeneo yao.

Toa Maoni Yako:
0 comments: