Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Gangwe Mob likiongozwa na Inspekta Haroun pamoja na Luteni Karama wakikamua vilivyo mbele ya mashabiki kibao waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya hivi sasa.
Wakazi wa Mbeya ni shangwe kwa kwenda mbele wakifuatilia makamuzi ya wasanii mbalimbali.

 Wasanii wa kundi la Uswahilini Matola wakikamua hivi sasa kwenye jukwaa ndani ya Uwanja wa Sokoine.
 Mmoja wa wasanii kutoka kundi la LWP,akiwapagawisha wakazi wa jiji la Mbeya waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Bongo 50,linadhaminiwa na kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel.
watu kibaoo afu ndioo kwaanza makamuzi yanaanza.

Pichani ni wakazi mbalimbali wa jiji la Mbeya wakiendelea kujitokeza kwenye tamasha la Bongo 50,ndani ya uwanja wa mpira wa Sokoine,tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel-Tanzania,kupitia huduma yao mpya walioizindua hivi karibuni kwa ajili ya wateja wao iitwayo Airtel Money.
Mkali wa muziki wa hip hop kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini,Mflame wa Rhymes ,Simba Mzee,Afande Sele akiwarusha vilivyo wakazi mbalimbali wa jiji la Mbeya,waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel,Airtel Money uliofanyika leo kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Sokoine.
 Wakazi wa jiji la Mbeya kutoka vitongoji mbalimbali wakishangilia vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha hilo la Airtel Money,lililofanyika katika uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Jaffarai akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya kutoka kampuni ya simu ya Airtel,ijulikanayo kwa jina la Airtel Money.
 Ilikuwa shangwe mwanzo mwisho,wakazi wa Mbeya wameipokea vyema huduma ya Airtel Money.
 Palikuwa hapatoshi leo kwenye uwanja wa Sokoine,jijini Mbeya.
Kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Temeke,Wanaume Halisi likiongozwa na kinara wao Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Sokoine,kwenye uzinduzi wa huduma mpya itolewayo na kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel,ijulikanayo kwa jina la Airtel Monye,ambapo wakazi wa jiji la Mbeya wameipokea kwa shangwe.
Jukwaani ni wakali wa miondoko ya hip hop katika muziki wa kizazi kipya,kulia ni Jaffarai pamoja na Jay Mo wakikamua vilivyo jukwaani kwenye tamasha la Bongo 50,lililodhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,kupitia huduma yao mpya ya Airtel Money.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: