...askari akijisogea eneo la tukio...
Majadiliano ya hapa na pale yalikuwa yakiendelea wakati wakipakia mwili wa marehemu kwenye gari tayari kwa kuupeleka hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Umati wa watu uliokuwepo eneo la tukio.
Hiki chumba ndicho ambapo amejipigia risasi askari huyo
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amejipiga risasi majira ya saa 1.30 usiku na kujiua akiwa katika lindo la benki ya National Microfinance (NMB House) iliyopo barabaya ya Jamhuri jijini Dar es Salaam.
Kajunason blog ilifika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu ukipakiwa kwenye gari ili upelekwe Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
---
Taarifa zilizotufikia hivi punde zimemtaja Askari Polisi aliyejiua kuwa ni mwenye namba G.347 PC David Peter Seleman mwenye umri wa miaka 23, aliyekuwa akifanya kazi kituo cha Kikuu cha kati jijini Dar es Salaam. PC David alikuwa ni miongoni mwa askari waliomaliza mafunzo ya awali ya polisi katika chuo cha Polisi (CCP) kwa sasa inafahamika Moshi Police Academy. Alimaliza mafunzo yake June 2009 na baadae kupangiwa Kanda ya Dar es Salaam.
Kabla ya kujiweka mtutu wa SMG mdomoni na kufyatua risasi moja na kufumua mdomo na kutokezea kwenye paji la uso, PC David alionekana akiranda randa huku na huko hali akipiga simu wa watu kadhaa na baadae kufuta kumbukumbu ya mawasiliano katika simu yake jambo ambalo ingawa itabainika alikuwa akiwasiliana na nani lakini pia Jeshi la Polisi kutumia muda wa ziada kupata mawasiliano hayo.
Mpaka sasa tayari Polisi wameshaanza kufanya upelelezi kujua chanzo cha askari huyo kujiua kwa kujipiga risasi. Askari huyo ametimiza idadi ya askari wanne kujiua kwa kujipiga risasi wenyewe ambapo Askari mmoja alijiua kwenye chuo cha Polisi DSM, mwingine wa kike alijiua Tarime na mwingine Iringa.

Kwa mujibu wa kauli za wenzake waliokuwa lindoni nae walisema kuwa, PC David alikuwa amekerwa na kupanda kwa posho za wabunge walizopandishiwa kutoka 70,000/- mpaka kufikia 200,000/- kwa siku wakati Polisi wao wanalipwa 100,000/- kwa mwezi mzima.
Mpaka sasa tayari Polisi wameshaanza kufanya upelelezi kujua chanzo cha askari huyo kujiua kwa kujipiga risasi. Askari huyo ametimiza idadi ya askari wanne kujiua kwa kujipiga risasi wenyewe ambapo Askari mmoja alijiua kwenye chuo cha Polisi DSM, mwingine wa kike alijiua Tarime na mwingine Iringa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: