Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na taka Singida, SUWASA, Marin Churi akifafanua jambo kwa ugeni ulioambatana na Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewj (kuhoto) pamoja na wengine walioambatana kwenye msafara huo wakiwemo viongozi wa siasa.
Mbunge wa Singida Mjini Mohammed Dewji akihoji juu ya mambo ya mradi wa maji mkubwa wa maji uliofadhjiriwa kwa msaada wa BADEA, kwa viongozi wa juu wa SUWASA.
Mkurugenzi wa SUWASA,Injinia Isaack Nyalonji Akitoa maelezo ya kisima kikubwa cha mradi wa BADEA katika eneo la Mwankoko, kushoto kwake Mbunge Mo Dewji alipotembelea kukagua mradi huo ambao unatarajia kumalizika mpaka Julai 12, mwakani. Wa pili kushoto, Mstahiki Meya, Shehe Salum Mahami, eneo la chanzo cha mradi huo wa maji.
Mbunge wa Singida Mjini,Mohammed Dewji akisalimiana na watendaji wakuu wanaosimamia mradi huo wa BADEA, Mr. Ragpathy (Contracts Manager) pembeni yake,Ashork Patel (Site Incharge) wa kampuni ya SPENCON SERVICE LTD.
Contract Manager wa kampuni ya Spencon Service Ltd, Mr.Ragpathy akimwelekeza Mo Dewji ramani ramani ya kamili ya mradi huo wa BADEA ambao unatarajia kumalizika mpaka Julai 12 mwakani.
Mo Dewji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa mradi huo wa BADEA ambao unatarajia kumalizika Julai mwakani.
Mo Dewji akihoji swali juu kwa wataalum wanaoshughulikia mradi huo usambazaji wa maji mjini maalufu kama BADEA, alipotembelea katika eneo hilo.
Tanki la maji likiwa kwenye hatu ya ujenzi likionekana kwa sasa ambapo ujenzi wake unatarajia kumalizika mwakani, ambapo mradi huo utakuwa na matumaini makubwa kwa wananchi wa Singida ukikamilika .
(Picha zote kwa msaada wa Mo blog team-www.mohammeddewji.com/blog).
---
Na Andrew Chale, Singida
MBUNGE wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji amesema ataendelea kuakikisha anapigania kumaliza tatizo la maji kwenye jimbo hilo ikiwemo kupambana nalo mpaka ngazi ya juu wakiwemo wanaokwamisha mradi huo.
Dewji alisema hayo mapema leo wakati alipotembelea mradi wa uboreshaji wa huduma za Maji Safi na Salama Singida Mjini unaofadhiri kwa ufadhiri mkubwa na Benki ya Kiarabu (BADEA) serikali na mashirika mengine yakiwemo Shirika la Mafuta ulimwenguni (OFID) unaogharimu dola za kimarekani bilioni 17.2 (SHILINGI 25,800,000,000,00) mpaka kukamilika kwake.
Alisema kua,mradi huo ambao ulianza kuombwa tokea miaka 10 iliyopita na kuja kukubaliwa mwaka 2009, umekumbwa na changamoto mbalimbali hali iliyopelekea kushindwa kukamilik a kwa wakati hivyo kuahidi kuonana na viongozi wa juu akiwemo Waziri mwenye dhamana na Rais ilikuondoa tatizo lililokuwepo.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Maji Singida (SUWASA) na kudai kua miongoni mwa changamoto hizo kwa mradi huo kupita kwenye sehemu za hifadhi ya barabara na katika makazi ya watu, suala hili linashughulikia kuona tunafika wapi ikiwemo kuonana na waziri mwenye dhamana” alisema Dewji.
Kwa upande wake Injiania Isaack Nyakonji wa SUWASA alisema mbali na matatizo ya mradi huo kupita kwenye hifadhi ya barabara na kazi ya watu, pia hali ya ukame na tatizo la umeme limechangia kusuaua kwa mradi huo.
“Singida ndani ya miaka miwili tulikua na ukame sambamba na ukatikaji wa umeme hali hiyo ilipelekea mradi huu kusimama.Pia mabadiliko ya gharama yamradi huu yameongezeka kutoka na mazingira kua magumu” alisema Inj.Nyakonji.
Katika ziara hiyo, Dewji alitembelea sehemu mbalimbali yamradi huo maalufu kama BADEA na kujionea utendaji wa kazi ikiwemo eneo la visima Mwankoko na sehemu ya tanki kubwa na la kisasa ambalo likikamilika litasaidia kupunguza shida ya maji Singida Mjini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: