Baadhi ya Wasanii wa Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Tip Top Connection.

Na Mwandishi Wetu
KUNDI la Tip Top Connection, limejipanga kuitikisa Dar mwishoni mwa wiki hii kwa kuwakutanisha wasanii wake wote ambao walishawahi kuwepo katika kundi hilo.

Akizungumza na Kajunason Blog kiongozi wa kundi hilo la TIP TOP Connections, Babu Tale alisema kuwa lengo la kuwakutanisha wasanii hao ni kuweza kunogesha zaidi na zaidi siku hiyo na kuzikonga  nyoyo za wapenzi wa burudani Bongo.

“Itakuwa shoo ya aina yake, nadhani haijawahi kutokea,” alisema Madee na kuongeza: “Kwa uhakika ni kwamba mastaa wote waliowahi kupita Tip Top watakuwepo na tutachangia jukwaa moja kupiga mzigo.

“Wasanii wote Z-Anto, MB Dog, Pingu, Keisha, Kasim na wengine wote waliopita Tip Top wataungana na sisi tuliopo, Tunda Man, Desso, Dogo Janja na wengineo kupiga shoo ya nguvu.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: