Hii ni foleni ya wananchi wa Mtwara walihangaika kupata mafuta hali imezidi kuwa tete ambapo mpaka sasa mkoa pekee unaoumia kwa kukosa mafuta ya petrol na diesel ni Mtwara, kwa mbeya, mwanza, Dodoma, arusha na mikoa mingine ambayo ilitajwa kwamba huenda kukawa na mgomo wa mafuta, hali ni shwari.
Mafuta Mtwara yamekauka kwenye vituo, na sasa hivi washkaji waliowahi kuyanunua kwenye vidumu wanauza lita moja kwa shilingi elfu tano, lakini jana wananchi walikuwa wakiuza vidumu wanauza lita moja kwa shilingi elfu nane.
Kwa sasa kituo pekee cha mafuta kilichokua kinauza hiyo bidhaa kimefungwa, na mmiliki hatoi sababu za kueleweka kwa nini amefunga ambapo kwenye foleni kituoni hapo, ukitaka kununua mafuta inachukua zaidi ya saa 6 mpaka saba kwenye foleni.
Toa Maoni Yako:
0 comments: