Mchambuzi wa Biashara (Business Analyst) wa kampuni ya Tigo, David Mugutti (wa pili kutoka kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na washindi wa promosheni ya “Kilimo Kwanza” waliojishindia Power Tiller Trekta mpya aina ya  VST SHAKTI MITSUBISH katika ofisi za Noble Motors jijini Dar es Salaam.Wengine ni Meneja Masoko wa Noble Motors, Max Mhagama (kulia),  washindi wa promosheni ya kilimo Kwanza, Macrine Charles (wa pili kutoka kushoto)  na Ediab Emil wa Chuo kikuu cha Ardhi  Dar es Salaam (kushoto).
 Mshindi wa Power Tiller Trekta aina ya VST SHAKTI MITSUBISH, , Macrine Charles (katikati) katika promosheni ya “Kilimo Kwanza” inayoendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi Tigo ikishirikiana na Noble Motors akiishukuru kampuni ya Tigo kwa kujishindia trekta ambayo itamsaidia katika kuendeleza kilimo. Wengine ni Mchambuzi wa Biashara (Busness Analyst) wa kampuni ya Tigo, David Mugutti (Kulia) na mshindi mwingine  na Ediab Amil wa Chuo kikuu cha  Ardhi  Dar Es Salaam (kushoto)
 Meneja Masoko wa Noble Motors, Max Mhagama (wa pili kulia) akimuelekeza mshindi wa Power Tiller Trekta, Macrine Charles jinsi ya kuliwasha Power Tiller Trekta alilojishindia kwa kupitia promosheni ya “Kilimo Kwanza” inayoendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi Tigo ikishirikiana na kampuni ya Noble Motors, jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko wa Noble Motors, Max Mhagama(wa pili kutoka kulia)  akimpongeza mshindi wa Power Tiller Trekta, Macrine Charles (kushoto) kwa kujishindia Trekta mpya aina ya VST SHAKTI MITSUBISH kutoka kampuni ya Tigo.Wengine ni muwakilishi kutoka kampuni ya Noble Motors (kulia), Mchambuzi wa Biashara (Busness Analyst) wa kampuni ya Tigo, David Mugutti (wa pili kutoka kushoto)
Meneja Masoko wa Noble Motors, Max Mhagama (wa pili kutoka kulia) akimkabidhi mshindi wa Power Tiller Trekta, Ediab Amil wa Chuo kikuu cha  Ardhi  Dar Es Salaam (kushoto) ambapo alishinda katika kushiriki katika promosheni ya “Kilimo Kwanza” inayoendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi Tigo ikishirikiana na kampuni ya Noble Motors,jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: