Mwakilishi wa Tigo Pamela Shelukindo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kukaribishwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maarifa Marieta Mlyalya.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Maarifa wakifurahia ujio wa wageni katika shule yao.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Maarifa wakiimba na kufurahia ujio wa wageni katika shule yao.
  Wanafunzi wa shule ya msingi Maarifa wakiimba na kufurahia ujio wa wageni katika shule yao.
Mwakilishi wa Tigo Pamela Shelukindo akimkabidhi madaftari ishara ya zawadi kwa mwalimu mkuu msaidizi Renatha Charles wa shule ya msingi Maarifa iliyopo Gongolamboto. Huku walimu pamoja na mwali mkuu wa shule hiyo akifurahia.
 Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maarifa iliyopo Gongolamboto jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyoo vilivyofanyiwa ukarabati na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maarifa Marieta Mlyalya akiwashukuru kampuni ya Tigo katika halfa ya kukabidhi ukarabati wa madarasa na vyoo uliofanyika shuleni hapo. Pembeni yake ni Mwakilishi wa Tigo Pamela Shelukindo pamoja na mwalimu mkuu msaidizi Renatha Charles.
 Makilishi wa Tigo ambaye ni afisa viwango wa Tigo Pamela Shelukindo akitoa ujumbe wa Tigo katika hafla fupi ya kukabidhi majengo yaliyokarabatiwa na tigo kufuatia kulipuka ka mabomu kulikotokea mwezi wa tano katika eneo la Gongolamboto na kuharibu majengo ya shule ya msingi Maarifa. Kutoka kushoto ni walimu mkuu msaidizi Renatha Charles, Pamela Shelukindo, Mwalimu Mkuu Marieta Mlyalya na  mwalimu mkuu msaidizi wa pili Tatu Kisemangu.
 Choo cha walimu kilichofanyiwa ukarabati.
 Mwakilishi wa Tigo Pamela Shelukindo akiongozana na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maarifa Marieta Mlyalya kukagua ukarabati uliofanyika katika choo cha walimu. Aliyesimama kwa nyuma ni mwalimu mkuu msaidizi Renatha Charles.
 Mwakilishi wa Tigo Pamela Shelukindo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maarifa iliyopo Gongolamboto vyoo vilivyofanyiwa ukarabati na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo katika majengo hayo huku tukio hilo likishuhudiwa na walimu wengine.
 Baadhi ya walimu waliohudhuria katika halfa hiyo.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imekabidhi darasa pamoja na choo kwa shule ya msingi Maarifa iliyopo eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam baada ya kumaliza ukarabati wa majengo ya shule hiyo yaliyoharibiwa na mlipuko wa mabomu yaliyolipuka katika kambi ya Gongolamboto jijini Dsm.

Akizungumza mara baada ya kukabithi rasmi majengo hayo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Afisa viwango na mwakilishi wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Pamela Shelukindo amesema “Sisi kama kampuni ya simu za mikononi ya Tigo tuliguswa kwa namna ya kipekee na tukio hili hasa ukichukulia kuwa wahanga wakubwa walikuwa ni watoto ambao walitaharuki na kuanza kukimbia huku na huko, na wengine kushindwa kwenda shule kutokana na mjengo kuharibika hali iliyowaondolea amani wakiwa shule”

Pamela akaongeza “Nadhani waandishi na wananchi wanaoipenda Tigo watakuwa ni mashahidi kuwa sisi tumekuwa mstari wa mbele katika kuchangia elimu hasa elimu ya msingi ambapo tumeweza kutoa vitabu na vibao vya mapajani siku chache zilizopita kwa baadi ya shule za msingi nchini kwani tunaamini watoto wakikua katika misingi yenye yenye uelekeo mzuri kielimu basi wao ndio watakaoijenga Tanzania nzuri siku za usoni”

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Maarifa Marieta Mlyalya akitoa shukrani zake kwa Tigo amesema “kwa niaba ya walimu, wazazi wa wanafunzi na wanafunzi wenyewe wa shule ya msingi Maarifa, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa msaada huu wa kutengenezewa madarasa haya mawili pamoja na choo. Tunashukuru kuona kwamba taasisi binafsi zinakuwa zinaguswa na matatizo yanayozikumba jamii inayozizunguka kwani hiyo inapunguza mzigo kwa serikali ambayo inafanya juhudi kubwa katika kuhakikisha inaleta maendeleo nchini.”

Mwalimu mkuu akaongeza pia kuwa  anafurahi kwamba Tigo wameweza kuwasaidia katika tatizo hilo la ukarabati wa majengo na kuziomba taasisi nyingine kuchangia sekta ya elimu katika shule mbalimbali kwani matatizo yanafanana nchini kote.

Mara baada ya tukio la mlipuko wa mabomu familia za maeneo yale zilipata misukosuko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupotezana kwa hofu, kuharibika kwa makazi na maeneo ya biashara, Tigo ilitembelea maeneo yale na kujionea jinsi uharibifu ulivyotokea na kuwapa mkono wa pole wahanga na namna ya pekee ikiwa ni pamoja na kuchukua jukumu la kukarabati majengo ya shule yaliyoharibiwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: