Mwakilishi wa Tigo Bw. Alex Msigara akiongea na Shule ya Msingi
Pugu Kajiungeni wakati wakukabidhi madarasa leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwalimu Mkuu Bi.
Mariam Korongo, kushoto kwake ni Afisa Elimu, Vifaa na Takwimu Ilala Bw. Abilah
Mchia.
Wanafunzi wa shule ya Msingi
Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam wakiimba kuwakaribisha wageni katika hafla ya kukabidhi madarasa leo.
Afisa Elimu, Bw. Abilah Mchia akiongea na waandishi wa
habari na walimu wakati Tigo wakikabidhi madarasa mawili ya Shule ya Msingi Pugu
Kajiungeni jijini Dar es Salaam.
Kulia kwake Bw. Alex Msigara wa Tigo na mwalimu mkuu Bi. Mariamu Korongo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Pungu kajiungeni ya jijini Dar es Salaam Bi. Mariamu Korongo akiongea na waandishi wa
habari na walimu wakati Tigo wakikabidhi madarasa mawili katika shule yake.
Mwakilishi wa Tigo Bw. Alex Msigara akiongea na
wanafunzi wa shule ya msingi msingi ya Pugu Kajiungeni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Pugu Kajiungeni wakishangilia.
Mwakilishi wa Tigo, Bw. Alex Msigara akimkabidhi mwalimu
mkuu wa shule ya Pugu Kajiungeni Bi Mariam Korongo, madaftari, kalamu za Tigo
pamoja na T-shirt.
Mwalimu
mkuu wa shule ya Pugu Kajiungeni Bi Mariam Korongo akionyesha madaftari, kalamu za Tigo
pamoja na T-shirt alizopewa zawadi.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekabidhi
madarasa mawili kwa shule ya msingi Pugu Kajiungeni iliyopo eneo la
Gongolamboto jijini Dar es salaam baada ya kumaliza ukarabati wa majengo ya
shule hiyo yaliyoharibiwa na mlipuko wa mabomu yaliyolipuka katika kambi ya
Gongolamboto mwezi May jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukabithi rasmi
majengo hayo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Afisa viwango na mwakilishi wa
kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Alex Msigara amesema “Sisi kama kampuni ya
simu za mikononi ya Tigo tuliguswa kwa namna ya kipekee na tukio hili hasa
ukichukulia kuwa wahanga wakubwa walikuwa ni watoto ambao walitaharuki na
kuanza kukimbia huku na huko, na wengine kushindwa kwenda shule kutokana na
mjengo kuharibika hali iliyowaondolea amani wakiwa shule”
Alex akaongeza “Nadhani waandishi na
wananchi wanaoipenda Tigo watakuwa ni mashahidi kuwa sisi tumekuwa mstari wa
mbele katika kuchangia elimu hasa elimu ya msingi ambapo tumeweza kutoa vitabu
na vibao vya mapajani siku chache zilizopita kwa baadi ya shule za msingi
nchini kwani tunaamini watoto wakikua katika misingi yenye yenye uelekeo mzuri kielimu
basi wao ndio watakaoijenga Tanzania nzuri siku za usoni”
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni Bi Mariam Korongo akitoa shukrani zake
kwa Tigo amesema “kwa niaba ya walimu, wazazi wa wanafunzi na wanafunzi wenyewe
wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa
msaada huu wa kutengenezewa madarasa haya mawili. Tunashukuru kuona kwamba
taasisi binafsi zinakuwa zinaguswa na matatizo yanayozikumba jamii inayozizunguka
kwani hiyo inapunguza mzigo kwa serikali ambayo inafanya juhudi kubwa katika
kuhakikisha inaleta maendeleo nchini.”
Mwalimu
mkuu akaongeza pia kuwa anafurahi kwamba Tigo wameweza kuwasaidia katika tatizo
hilo la
ukarabati wa majengo na kuziomba taasisi nyingine kuchangia sekta ya elimu
katika shule mbalimbali kwani matatizo yanafanana nchini kote.
Mara baada ya tukio la mlipuko wa mabomu familia
za maeneo yale zilipata misukosuko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupotezana kwa
hofu, kuharibika kwa makazi na maeneo ya biashara, Tigo ilitembelea maeneo yale
na kujionea jinsi uharibifu ulivyotokea na kuwapa mkono wa pole wahanga na
namna ya pekee ikiwa ni pamoja na kuchukua jukumu la kukarabati majengo ya
shule yaliyoharibiwa.
Hongereni sana Tigo kwa kuwa msitari wa mbele katika kuisaidia jamii
ReplyDeleteTigo oyeeeeeeeeeeeeeeeee!
ReplyDeleteHongereni sana japo mtandao wenu kama kwa sasa umezidiwa
ReplyDeleteMambo ya Tigo hayo, hongereni kwa kuwasaidia vijana wetu
ReplyDeleteWanafunzi wanaoneka wanafuraha sana
ReplyDelete