MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua, Tawi la Benki ya Diamond Trust (DTB) katika makutano ya barabara ya Lupa na Soko, jijini Mbeya.
Baadhi ya wateja waliohudhuria katika ufunguzi wa tawi la Benki ya Diamond Trust lililopo jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Diamond Trust Benki (DTB), Abdu Samji akiwa na MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama (wa kwanza kutoka kulia) pamoja na wakurugenzi ya benki hiyo.
---
Tawi la kumi na tatu la Benki ya Diamond Trust lililopo makutano ya Barabara za Lupa na Market limefunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro
Mh Kandoro katika uzinduzi huo aliipongeza Banki hiyo kwa kubuni tawi lenye taswira ya kipekee na kujikita katika kuwezesha sekta ya biashara ndogo na za kati yaani SME kupitia mtandao wa matawi unaokua wa Benki hiyo. Mh Kandoro ametoa rai kwa mabenki zaidi kufungua matawi yake Jijini Mbeya ili kutoa mchango katika kueleza maendeleo ya kiuchumi Jijini Mbeya, DTB ni benki ya kumi kufungua tawi katka Jiji la Mbeya.
Mh Kandoro alisema kupanuka kwa Benki ya Diamond Trust ni kiashia bayana cha umakini na uwajibikaji wa benki hiyo katika kuwafikia wananchi wa Tanzania. Aliipokeza benki ya DTB kwa kuwa na masaa zaidi ya kutoa huduma kwa wateja wake kulinganisha na mabenki yaliopo Jijini Mbeya ambayo anaamini itatoa unafuu na nafasi zaidi kwa wateja kupata huduma za kibenki
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Ndg Abdul Samji katika hotuba yake ya kumkaribisha Mheshimiwa Kandoro alisema tawi la mbeya ni tawi la kwanza la Benki hiyo kwa mikoa ya kusini na ni kithibitisho cha utekelezaji wa malengo ya Benki ya DTB kufungua matawi katika mikoa mikubwa ya Tanzania. Benki hiyo inatarajia kuongeza wigo wa matawi yake Moshi, Iringa, Morogoro, Shinyanga na Kahama hii ikiwa ni pamoja na kufungua matawi ya ziada katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza kwa kipindi kifupi kijacho
Ndg Samji alisema tawi la DTB Mbeya limelenga katika kuwezesha wafanya biashara wa jiji la Mbeya kwa kuwaunganisha na wigo mpana wa Benki lakini nchini ikiwa ni pamoja na mtandao katika Nchi za Kenya, Uganda na Burundi ambapo Benki ina matawi yake. Benki itakuwa ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa watu binafsi na wafanyabiashara kuanzia saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni kwa siku za juma na kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa saba mchana kwa siku za jumamosi. Huduma za kupokea na kutuma fedha kupitia Western Union na huduma za kadi za VIZA za kimataifa kwa malipo na kutolea fedha kama baadhi ya huduma zinazotolewa na Benki ya Diamond Trust.
DTB ina matawi 13 Nchini; 6 katika mkoa wa Dar es Salaam, 2 Arusha na moja katika kila mikoa ya Tanga, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Unguja- Zanzibar. Hivi karibuni Benki itafungua tawi jipya lililopo Masaki Dar es Salaam na Moshi mjini ikiwa ni sehemu utekelezaji wa mpango wake kufikia mikoa zaidi Nchini. Benki ya DTB inatoa huduma za kibenki katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi yenye jumla ya matawi 68 Afrika Mashariki.
DTB ni mshirika wa Mfuko wa maendeleo wa Aga Khan (AKFED) ambao ni shirika la kiuchumi la mtandao wa maendeleo wa Aga Khan (AKDN).
Hongereni DTB kwa kuvuka hatua
ReplyDeleteHongereni DTB kwa kuvuka hatua
ReplyDelete