Tarehe 24 Novemba 2011, Dar es Salaam. Tigo mtandao unaoongoza Tanzania kwa kutoa huduma za mawasiliano kwa bei nafuu unasheherekea kufikisha wateja 20,000 ambao wamejiunga katika mtandao wake wa kijamii wa facebook kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wapenzi na watumiaji wa mtandao huo.

“Tunafurahi kuona kuwa mtandao wetu wa mawasiliano wa kijamii wa facebook umefikisha idadi hiyo, kwetu sisi ni mafanikio makubwa,” alisema Diego Gutierrez Naibu Meneja Mkuu wa Tigo. “Wateja wetu ni muhimu sana katika kutoa ushirikiano kuendelea kutumia mtandao wa mawasiliano wa kijamii wa facebook na tutaendelea kushirikiana nao kwa karibu,” alisema.

Kwa kuonyesha kuwajali wateja wake Tigo inatoa zawadi kuwapa meseji tatu za bure na muda wa dk. 2 za bure za maongezi kwa muda wa siku 20 mfululizo. Zawadi zitakuwa zinapatikana katika vifurushi vya mauzo. Lakini Tigo itatoa zawadi hizo bure kwa wale watakaojaza fomu za kushiriki. Watumiaji wote wa mtandao huu wa kijamii hawana budi kujiunga zaidi ili kujishindia zawadi mbali mbali kwa kujaza maelezo yao kupitia http://www.facebook.com/TigoTanzania.

Pamoja na kujiunga na mtandao wa facebook wa Tigo pia watumiaji wa mtandao wanaweza kuwafahamisha watu wengine juu ya promosheni hii kwa kubonyeza neno ‘Share’ ambalo liko eneo la chini kabisa katika ukurasa wa mtandao huo kwa kuwafahamisha ndugu na jamaa kushiriki katika promosheni hii. Kwa jinsi mtumiaji atakavyoweza kuwaunganisha watu wengi ndivyo atakavyowawezesha kushinda zawadi.

Promosheni hii inaendelea mpaka hapo watumiaji wa facebook watakapofikia idadi ya 25,000. Facebook hii ni kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo tu wa hapa Tanzania. Kila mtumiaji au mpenzi wa mtandao huu atakayejaza fomu ya kushiriki atazawadiwa mwishoni mwa promosheni hii.

Tigo pia iko katika mchakato wa kuja na stahili mpya ambayo itakuwa ikitumika katika mtandao wake wa kijamii wa facebook kuwapa uzoefu zaidi wapenzi na watumiaji wa Tigo facebook.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: