Waumini wa kituo chicho cha maombi wakimsaidia mgonjwa huyo kupanda katika kitanda ili kupimwa baada ya kuamka akiwa Mochwari
Hapa mgonjwa huyo akishushwa katika gari baada ya kutolewa Mochwari
Wasamaria wema wakiwa wamesimama nje ya chumba cha daktari kusubiri majibu huku mke wa marehemu akiwa amekaa chini.
   Mauaza uza yaibuka mjini Iringa baada ya mgonjwa ambaye alifika kufanyiwa maombi kwa mmoja kati ya wahubiri maarufu mkoani Iringa kukata kauli yake akiwa nje ya ukumbi huo maarufu wa maombi mjini hapa na baada ya kufikishwa chumba cha kuhifadhiwa maiti (Mochwari) katika hospital ya mkoa wa Iringa maiti hiyo iliamuka na kupelekea ndugu kuupeleka mwili huo kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mke wa mgonjwa huyo Amina Ramadhan alisema kuwa mme wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya jana mgonjwa huyo kuomba kuletwa mjini Iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani Iringa Boaz Sollo wa kituo cha maombezi cha overcomers.

Hata hivyo alisema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mgonjwa huyo aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa Mochwari ghafla marehemu aliamuka na kuanza kurusha rusha mikono yake hali iliyopelekea kurudishwa tena mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kumtaja mjane wa marehemu Bi Amina Ramadhan alimtaja marehemu kuwa ni Gerald Tadei Ngusi

Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa na hadi mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.


Picha na habari kwa hisani ya Francis Godwin Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: