JESHI la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mwanamke mmoja Fatuma Mwakachingo pamoja na mume wake Mogela Victory kwa tuhuma za kupatikana na viungo vya binadamu na vitu vingine vyenye imani ya kishirikina.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Adolphina Chialo alisema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 29 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi katika mtaa wa Zaire Wami Dakawa Wilaya ya Mvomero mkoani humo.
Kamanda Chialo alisema kuwa mwanamke huyo ni mganga wa kienyeji na kwamba alikamatwa pamoja na mume wake baada askari kupekua katika nyumba waliyokuwa wakiishi na kufanyia shughuli za kiganga ambapo viungo hivyo pamoja na vitu vingine vyenye imani za kishirikina vilikamatwa.
Kamanda Chialo alivitaja viungo hivyo kuwa ni kichwa cha binadamu, ngozi ya binadamu, magamba ya konokono na vitu vingine ambavyo vinaaminika kuwa ni vya kishirikina na inadhaniwa kuwa alikuwa akivitumia katika shughuli zake za uganga.
Alisema kuwa polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupewa taarifa kutoka kwa raia wema ambao walieleza kuwepo kwa viungo hivyo ndani ya nyumba hiyo.
Aliongeza kuwa kamanda huyo alisema kuwa baada ya kukamatwa watuhumiwa hao wameshachukuliwa maelezo na walifikishwa mahakamani Novemba 1 kujibu mashitaka yatakayowakabili.

Toa Maoni Yako:
0 comments: