KAMANDA WA POLISI MKOA WA MOROGORO ADOLPHINA CHIALO. |
Na Venance George, Morogoro.
TAKRIBANI wiki moja ikiwa imepita baada ya baadhi ya askari polisi wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kutuhumiwa kujihusisha na mtandao wa ujambazi, kashfa nyingine imelikumba Jeshi hilo, likituhumiwa kushirikiana na wafanya biashara wakubwa wanaojihusisha na madawa ya kulevya.
Mmoja wa askari wa Jeshi hilo hivi karibuni alitoa tuhuma nzito kupitia vyombo vya habari kuwa baadhi ya askari wa kitengo cha kuzuia ujambazi wamekuwa wakihusika na mtandao huo tuhuma ambazo zimemfanya askari huyo kukamatwa na kuwekwa ndani kwa madai ya kutoa taarifa zisizo sahihi.
Hata hivyo kashfa ya hivi sasa imetolewa na mzazi wa mwanafunzi (JINA LIMEHIFADHIWA) anayesoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Morogoro, (JINA TUNALO), ambaye alishutumu jeshi hilo kwa kushindwa kuwakamata wafanyabiashara sita wa madawa ya kulevya wa mjini hapa ambao wamekuwa wakimtumia mtoto wake huyo katika kusafirisha na kuuza madawa ya kulevya.
Mtumishi wa shule ya sekondari ya Morogoro, alitoa tuhuma hizo mbele ya waandishi wa habari huku akidai kuwa tuhuma hizo amekwisha zifikisha katika vyombo mbalimbali vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi,ofisi ya Usalama wa taifa ,Ofisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) pamoja na kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya nchini lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Akielezea kuhusu mkasa wa mtoto wake kushirikishwa katika mtandao huo wa madawa ya kulevya,alisema alianza mwezi april mwaka huu baada kutoweka nyumbani kwa kipindi cha wiki mbili na nusu na kurudishwa nyumbani na dereva wa taksi akiwa ameonekana kulewa madawa ya kulevya hali ambayo iliwatia mashaka.
“ Tulimuhoji huyo dereva wa taksi alikompata huyo kijana wetu,alituambia alimuokota katika eneo la masika katikati ya mji wa Morogoro akiwa hajitambui ,tulimchukua na kumpeleka hospitali kwajili ya kupatiwa matibabu’’ alisema Gando.
Alisema kuwa wiki tatu baadaye kijana wake alitoweka tena katika mazingira ya kutatanisha na kuonekana na watu wanaodhaniwa kujihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya mkoani Arusha baada ya kupewa taarifa na mmoja wa aliyekuwa mwanafunzi wake wakati akisoma katika shule ya sekondari Morogoro.
Mzazi huyo alisema baada ya kupata taarifa hiyo,alilazimika kumpigia simu ndugu yake aliyeko arusha ambaye anafanya kazi katika kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya kwajili ya kumfatilia hata hivyo wakati jitihada hizo zikiendelea mtoto huyo alirudi nyumbani kwao mjini morogoro .
Alisema kuwa waliamua kumpeleka kituo kikuu cha Polisi mkoa wa morogoro kwajili ya kuhojiwa ambapo alitaja majina ya watu wanaomtumia katika biashara ya madawa ya kulevya kuanzia Morogoro mpaka Arusha mbele mkuu wa Polisi wa wilaya pamoja baadhi ya askari.
Orodha ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya waliotajwa kumtumia kijana huyo inahusisha watoto wa wafanyabiashara maarufu katika mkoa wa Morogoro pamoja na mmoja wa ndugu wa kigogo mstaafu wa Jeshi la Polisi ambao majina yao kwa sasa yameifadhiwa.
Mzazi huyo alieleza kushangazwa na Jeshi la polisi katika mkoa wa Morogoro mpaka sasa kutochukua hatua zozote kwa wahusika walitajwa katika orodha hiyo na kwamba hivi sasa mtoto huyo ametoweka tena na kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa wahusika waliotajwa .
Alisema kuwa licha ya suala hilo kulifikisha katika vyombo vya usalama lakini alishawai kulifikisha katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye alimuelekeza kamanda wa Polisi kulishughulikia suala hilo lakini mpaka leo halijapatiwa ufumbuzi na kuhisi kuwa kuna harafu ya rushwa kwakuwa wahusika waliotajwa kuunda mtandao huo wanafahamika .
“Ninahisi kuna harufu ya rushwa au baadhi ya askari wanashirikiana na hao wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ,kwanini watu hao licha ya kutajwa hadharani lakini hawajakamatwa, kwani wengi wao wanafahamika na wamekuwa wakijihita marais wa sehemu wanazokaa “alisema Gando kwa uchungu.
Akizungumzia shutuma hizo nzito, Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Joseph Rugila,alikiri jeshi hilo kupokea majina ya watu wanoojihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Morogoro baada ya kumhoji kijana huyo,na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wake.
“Tuhuma za madawa ya kulevya nzito na zinazofanywa kwa siri kubwa na hivyo inahitaji ushahidi wa kutosha ili kuthibitisha ukweli wa madai hayo vinginevyo unaweza kumtuhumu mtu lakini ukakosa ushaidi” alisema Rugila.
Naye kamanda wa takukuru Mkoa wa Morogoro, Stella Mpanju,alikiri kupokea taarifa hizo kupitia mzazi wa mwanafunzi huyo na kudai kuwa, maafisa wake wanaendelea kulifanyia kazi kubaini kama kuna rushwa imefanyika mpaka watuhumiwa wanachelewa kukamatwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments: