mmmm
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akifafanua jambo wakati wa mahojiano katika redio Clouds Fm iliyopo jijini Dar es Salaam. Pembeni yake yupo mtangazaji wa Clouds Fm Wasiwasi Mwabulambo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akifafanua jambo wakati wa mahojiano katika redio Clouds iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds Fm Wasiwasi Mwabulambo akijaribu kuwaonyesha Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Afisa Habari wa wizara hiyo Mindi Kasiga jinsi redio inavyofanya kazi online wakati wlipohudhuria katika mahojiano.
 Mtangazaji wa Clouds Fm, Paul James akijaongea na Waziri Membe.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akifafanua jambo kwa mapana. Pembeni yake yupo mtangazaji wa Clouds Fm Paul James.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akifafanua jambo wakati akifanyamahojiano na Clouds Tv huku Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba akifuatilia wa makini.
Afisa Habari wa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga (kulia) akifafanua jambo mbele ya Waziri Membe (kushoto) kati ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba pamoja na Simalenga Simon ambaye ni Produder wa redio Clouds Fm.

Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati alipotembelea Clouds Media Group.
----
Tanzania ni nchi ya kuigwa- Waziri Membe

Watanzania wametakiwa kuuenzi Umoja, Upendo na Mshikamano ulipo Tanzania maana ndiyo sifa inayoiweka nchi katika historia.

Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati akifanya mahojiano katika redio Clouds iliyopo jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa nchi za jirani wanatamani sana amani iliyopo mchini Tanzania, maana nchi nyingine huwa mpaka wapigane ndiyo amani ipatikane.

"Tanzania tunaonewa wivu kuhusu huu utaratibu wa kupeana vijiti vya uongozi, kijiti cha Mzee Nyerere akamkabidhi Mwinyi kwa amani na kura...kijiti cha Mzee Mwinyi akamkabidhi Mkapa na vile vile kijiti cha Mkapa akamkabidhi Kikwete hivi ndivyo inavyopaswa kufanyika siku zote," aliongezea Waziri Membe.

"Tunaposherehea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania ni vyema tukatambua kuwa Tanzania ni nchi ya pekee na ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: