Baadhi ya matrekta yaliyotayarisha katika kazi ya kuburuga katika matayarisho ya kilimo cha mpunga katika Bonde la mpunga la Cheju, Wilaya ya Kati Unguja kwa msimu wa 2011-2012.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia viongozi wa jumuiya za wakulima katika bonde la cheju alipowasili kuzindua kilimo hicho kwa msimu wa mwaka 2011-2012, katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya kati Mkoa wa  Kusini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiyakagua  matrekta ya wizara ya Kilimo na maliasili, wakati wa uzinduzi wa kilmo cha mpunga katika bonde la cheju  Wilaya ya Kati Unguja,jana kabla ya kuzindua rasmi  kilimo hicho kwa msimu wa mwaka 2011-2012.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasha Trekta kama ishara ya uzinduzi wa kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012, katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya katika  Mkoa wa  kusini Unguja.
 Baadhi ya matrekta yakianza kuchimbua katika hatua za matayaarisho ya kilimo cha mpunga katika bonde la Cheju, kwa mwaka 2011-2012 kilichozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, jana katika bonde hilo Wilaya ya kati Unguja.
 Mwakilishi wa Jumuiya za wakulima katika bonde la cheju Getruda Adolfi Mkude, akisoma risala ya wakulima katika uzinduzi wa kilimo cha mpunga kwa msimu huu wa mwaka 2011-2012, ambapo wastani wa ekari elfu tatu zitalimwa mpunga kwa kutumia mbegu za kisasa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wakulima wa bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya Kati Unguja, baada ya  kuzindua matayarisho ya kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012, katika  Mkoa wa  kusini Unguja.
Wakulima waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa kilimo cha mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012, katika bonde la Cheju Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wakulima hao naa kuwataka kutumia mbegu bora za kisasa ili kukuza pato katika kilimo hicho.

 Picha na Ramadhan Othman IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: