Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea Trailer ya Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.

Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka  Kutoka Urban Pulse na yatarushwa Hewani kupitia  kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30 octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.

Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.

Asanteni,

Urban Pulse Creative.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: