Mwakilishi wa Tigo Matiko Elliya akimkabidhi vitabu Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Fatma Ally wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu 1200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 kwa shule ya msingi ya Kilimahewa.
 Gwaride rasmi lililoandaliwa na wanafunzi wakakamavu wa shule ya msingi Kilimahewa likipita kwa heshima mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kukabidhi vitabu 1200 kwa shule hiyo. Kutoka kushoto mstari wa mbele waliosimama ni Makamu mkurugenzi wa halmashauri ya Nanyumbu Justin Lukaza, Afisa Utawala wa Tigo mkoa wa Lindi Matiko Elliya, Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Fatma Ally, Meneja uhusiano Tea Sylivia Lupembe na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kilimahewa Adolf Katambo.
Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Fatma Ally akifurahia vitabu na kuwaonesha wazazi, walimu na wanafunzi waliofika katika hafla ya kukabidhi vitabu ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kupitia kampeni yake ya Tigo tuChange ilikabidhi vitabu 1200 kwa shule ya msingi Kilimahewa.
---
Katika jitihada za kuendelea kuchangia elimu nchini, kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imekabidhi vitabu kwa shule ya msingi ya Kilimahewa iliyopo wilayani Nanyumbu, Mtwara kupitia kampeni yake ya “Tigo tuChange” ambapo vitabu vy Kiswahili, kiingereza hesabu, uraia tehama na masomo mengine vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 vimetolewa. 

Shule ya msingi ya Tuangoma ya jijini DSM ndio iliyofungua mlango wa kampeni ya Tigo tuChange ambapo shule ya msingi Kilimahewa iliyopokea vitabu hivyo leo hii imekuwa ya tano nay a mwisho kwa kampeni hii. Tigo iliendesha kampeni hii ya tigo tuchange tarehe 9 July 2011 ambapo wateja waliweza kuchangia kampeni hii ya Tigo tuChange ndani ya saa moja saa tatu mpaka saa nne asubuhi. Tigo iliweza kukusanya fedha taslim ya shillingi 25,930,160 ambazo ndizo zilizotumika kununulia vitabu. 

Akielezea madhumuni ya kampeni ya Tigo Tuchange wakati wa kukabidhi vitabu katika shule hiyo, Afisa utawala wa Tigo, mkoa wa Lindi Matiko Elliya amesema Tigo ni sehemu ya jamii na kwa jamii yoyote ili iweze kuendelea elimu iliyobora ni nguzo muhimu, na kwa kutambua hilo ndio maana Tigo imeamua kuchangia elimu kupitia vitabu. 

Matiko akaongeza pia “Tigo imeguswa na idadi ya matatizo ambayo yanayowakabili katika shule za msingi nchini Tanzania na tumegundua kwamba uhaba wa vitabu ni moja wapo ya matatizo haya makubwa yanayosababisha kutolewa kwa elimu isiyokuwa na viwango na hivyo ufaulu kwa wanafunzi umekuwa si wa kuridhisha. Kwa sasa tumeweza kuipatia shule hii zaidi ya vitabu 1,200 ambavyo vinathamani ya zaidi ya shillingi millioni tano. Vitabu hivi vipo katika mgawanyo sawia katika masomo mbalimbali kama jiografia, hisabati mpaka sayansi. Tunaamini kwamba kila mwanafunzi akiwa na kitabu chake ataweza kuwa makini darasani na badaaye kuweza kufaulu katika mitihani yake. 

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kilimahewa iliyopo Masasi, Mtwara bwana Adolf Katambo alisema kwamba wamefurahi sana na kazi ya Tigo kwa kugawa vitabu na kwamba wameisaidia shule hiyo sana kwa vile kuna matatizo mengine na kama alivyosema mwakilishi wa Tigo kwamba sasahivi watoto hawa wataweza kusoma vizuri darasani kabla ya hapo ilibidi watoto 3 mpaka 5 wagawane kitabu kimoja.

Mwalimu mkuu aliongeza kwakusema kwamba shule hiyo inapambana na matatizo mengi na serikali haiwezi kutatua matatizo yote kwahiyo anafurahi kwamba Tigo wameweza kusaidia kuwasaidia katika tatizo moja ambayo ni uhaba wa vitabu na pia mwalimu mkuu alisema kwamba angependa makampuni mengine waige mfano wa Tigo. 

Matiko Elliya aliongeza kwamba uaminifu na upendo uliyoonyeshwa kwa Tigo imewafanya Tigo warudi kutoa kwa jamii, “ WaTanzania wametupa ushirikiano na tunaona kwamba ni wajibu wetu kutoa kwa jamii. Hii ni mwanzo tu wa kuwasaidia wa Tanzania na changamoto katika sekta ya elimu na tuna mpango wakuendelea hapo badaaye katika sekta ya elimu 

Naye mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Fatma Ally amesema amefurahishwa sana na msaada huo ambao umeifikia shule inayoongoza kwa elimu wilayani kwake licha ya uhaba mkubwa wa vitabu unaoikabili na kuzitaka taasisi nyingine binafsi na za serikali kuchangia katika elimu na hasa kuiga mfano huu ambao kampuni ya simu za mkononi ya tigo imeuweka. Kama alivosema afisa uhusiano wa TEA kwamba tunawaomba Tigo kwamba hii isiyo mwisho wa Tigo kutoa msaada katika sekta ya elimu tunategemea kwamba Tigo itaendelea kutoa msaada. Pia tunawahamasisha taasisi na ma kampuni wengine waige mfano ya Tigo Tanzania.  

Akiongea kwa niaba ya Mamlaka ya elimu Tanzania TEA, Silvia Lupembe amesema anafurahia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia sekta ya elimu. ‘Hatua hii ni nzuri na yenye manufaa kwa Taifa kwani vitabu vimeendelea kuwa tatizo kubwa katika sehemu mbalmbali ndani ya nchi na hivyo tunaishukuru tigo kwa kutufuata na kutaka ushiriki wetu katika kampeni hii na tungependa mashirika na taasisi binafsi na za serikali kuiga mfano huu wa Tigo katika kuchangia elimu ili tuweze kuhakikisha watoto wanapata nyezo muhimu za kujifunzia wakiwa shuleni”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: