Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu akisalimiana na Viongozi
wa Kampuni ya SS BAHKRESA mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi ya
kutembelea viwanda vya kampuni hiyo na kujionea uzalishaji wa chakula
unaofanywa na kampuni hiyo.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu(Kushoto) akisikiliza
maelezo ya utendaji wa kampuni ya SS BAHKRESA kutoka kwa Afisa Mtendaji
wa Kampuni hiyo Bw Hussein Sufian.
Mkuu
wa Kitengo cha Uzalishaji wa Kampuni ya SS BAKHRESA Bw Patrick
Muriuki(Mwenye Kofia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Lazaro Nyalandu(Mwenye suti) kuhusu aina mbali mbali za unga wa
ngano zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu ( Kulia) na Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Viwanda kastika Wizara ya Viwanda na Biashara Eng
Marwa(Kushoto), wakionja kinywaji kipya kinachozalishwa na kampuni ya SS
BAHKRESA.
---
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, ameipongeza kampuni
ya SS BAHKRESA kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwa dhati katika uzalishaji
wa bidhaa za chakula za aina mbali mbali.
Mh Nyalandu ametoa ponghezi hizo Jijini Dar es salaam mara baada ya ziara yake kutembelea viwanda vya kampuni hioyo ili kujionea hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa za chakula unaofanywa na kampuni hiyo.
“Ndugu zangu ninawapongeza sana kwa kazi iliyotukuka ambayo mnaifanya kwa miongo kadhaa sasa, juhudi zenu zipo dhahiri, mnagusa maisha ya Watanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Vyakula na Vinywaji mavyozalisha sio tu vinalinda afya zetu, bali pia ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana, serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kila linalowezekana” amesema Nyalandu.
Mh Nyalandu ameiomba kampuni hiyo kuwa tayari kuwafundisha na kuwaonesha njia wajasiriamali wadogo ili nao washiriki kikamilifu katika kuzalisha bidhaa za chakula kwa ubora unaokubalika huku akisisitiza umuhimu wa vyakula hivyo kuuzwa kwa bei nafuu ambnayo watu wote watamudu.
Pamoja na kushiriki katika kilimo cha mazao mbali mbali ambayo ni malighafi kwa viwanda vyake,
yanayozalishwa kwa wingi kote nchini na pia ni miongoni mwa kampuni zilizoajiri idadi kubwa
ya Vijana.
SS Bahkressa ni wanunuzi wakubwa wa mazao mbali mbali na matunda nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments: