Na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi Kigoma

Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Buronge mjini Kigoma, wamefariki dunia baada ya roli walilopanda kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba udongo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja wanafunzi hao kuwa ni Mussa Ibrahimu(16) na Yusuph  Ismai(16), wote ni wanafunzi wa darasa la sita katika shuleni hapo.
 Kamanda Kashai amesema kuwa tukio hilo limetokea  majira ya Saa 12 jioni jana huko kwenye eneo la Nkema mjini Kigoma na miili ya marehemu hao ilifukuliwa na kukabidhiwa kwa ndugu zao kwa shughuli za mazishi.
 Kamanda kashai ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto waliopo chini ya umri wa miaka 18 wanazingatia masomo na kuacha kufanya kazi za kujipatia kipato zikiwemo hizo za uchimbaji mchanga ambazo ni hatari kwa maisha yao.

Amesema shughuli kama hizo pia zinapunguza maendeleo ya mtoto shuleni na ni kinyume cha sheria na haki za mtoto.

Katika maeneo ya Nkema kuna uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji udongo unaotumika kwa kujengea nyumba mjini humo na ameziomba mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya wale wote wanaoharibu mazingira kwa kisingizio cha kujitafutia kipato. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: