Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
 
Jeshi la Polisi Zanzibar limeanza kupitia upya na kuratibu kero, malalamiko na madai mbalimbali ya askari wa Jeshi hilo na kuhakikisha utekelezaji wake.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi Zanzibar SACP Keneth Kaseke, wakati wa mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Shamsis Vuai Nahodha mjini Zanzibar.

Kamanda kaseke, amesema kuwa utaratibu huo utawawezesha Askari wa Jeshi hilo wenye malalamiki na madai ya msingi, kupata haki zao wanazostahili na kujenga imani na Serikali yao.

Kwa muda mrefu sasa baadhi ya Askari Polisi waliokuwa na kero na madai mbalimbali walikata tamaa na kukosa uhakika wa kama kweli madai yao yalikuwa yakishughulikiwa tofauti na walivyopata uhakika wa kuabnza kulipwa kwa baadhi ya malimbikizo ya madeni yao pamoja na ufafanuzi wa Kamanda Kaseke.

Katika mkutano huo, Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya nchi, aliwaagiza Makamanda na Maafisa mbalimbali wa Jeshi hilo, kuhakikisha kuwa wanaendelea kusimamia kwa makini na kulinda maslahi ya askari waliochini yao.

Waziri Nahodha amesema kuwa anaungana na kauli ya Kamanda Kaseke ya kuangaliwa upya kero na malalamiko ya askari hao kama sehemu ya kuwatia moyo na kuwaongezea ari ya kiutendaji katika kazi zao.

Amesema Askari wengi wa Jeshi hilo wamekuwa wakifanya kazi zao vizuri na kwa moyo wa dhati na kwamba baadhi yao wamekuwa wakikatishwa tama na kuwavunja moyo na baadhi ya viongozi.

Amesema kuna baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakiwakatisha tama askari na hata kutowasikiliza shida zao zikiwemo zile za binafsi na za kikazi jambo amblo amesema limekuwa likiwakatisha tama kazika utendaji wa kazi zao.

Katika Mkutano huo, Waziri Nahodha aliwahakikishia Askari kao kuwa kila mwenye dai na lalamiko la msingi atasikilizwa na kupatia mrejesho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: