Na Andrew Chale, Bagamoyo

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Emmanuel Nchimbi anatarajia kufunga tamasha la 30  Octoba Mosi na kutoa vyeti kwa wahitimu mbalimbali wa chuo cha sanaa Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,Mkuu wa sehemu ya tamasha  na maonyesho chuoni hapo,Abraham Bafadhir 'Bura' alisema kua tamsha hilo lililoanza Septmba 26, linatarajia kumalizika Octoba Mosi  na waziri Nchimbi.

"Tamasha limepamba moto na Oktoba Mosi linafungwa rsmi na waziri mwenye dhamana,Nchimbi pia atatoa vyeti kwa wahitimu mbalimbali waliomaliza mwaka wa tatu chuoni hapo" alisema Bura.

Pia alisema kua vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni vya kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na vile vya nje ya Tanzania vimetoa burudani na vingine vikiendelea kutoa mpaka hapo siku mwisho.

Aidha, alisema kua,mpaka kufikia mwaka huu wa 30, ni wakati sasa wa wadau kujitokeza na kutoa ufadhiri ilikua la kimataifa zaidi. "Tunaomba wadhamini waje kwa wingi kudhamini ilikua tamasha la kimataifa kama yalivyo matamsha mengine, hapa ndipo taaluma ya sanaa ya asili,utamaduni na kisasa ya kila aina inazaliwa hapa hivyo ni changamoto kwa wadau kujitokeza sasa ilikutimiza malengo" alimalizia Bura.

Vikundi vitakavyotumbuiza leo kwenye tamasha hilo amblo linabeba umati mkubwa wa wananchi wa Bagamoyo na wageni mbalimbali mjini hapa ni pamoja na Kizingo Art (Kenya), Alain Izai (Congo DRC), Buyegu Theatre group (Mwanza-Tanznaia) na Beatrice Taisamo(TaSUBa-Chuo cha Sanaa Bagamoyo) na vingine vingi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: