Stella Aron na Mohamed Hamad
SERIKALI imeombwa kuangalia kwa upana suala la mchakato wa uandaaji wa katiba mpya kwa kuweka kifungu kitakachowasaidia mashoga kuondokana na adha na kero ya kunyanyapaliwa.
Ombi hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Bw. Abdul Zungu ambaye ni shoga na mwanaharakati katika tamasha la jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Alisema kuwa kutokana na hali waliyonayo asilimia watu wengi katika jamii wamekuwa wakiwatenga na kuwanyanyapaa na kusababisha kuishi kwa hofu na hata kutishiwa kuuawa kwa silaha.
Alisema pia wapo baadhi ya mashoga waliopoteza maisha kutokana na kuuawa na wanapofuatilia huwa kesi zao hazitiliwi maanani kutokana na kukosa utetezi.
"Tuna haja ya sisi kupata mwakilishi katika ngazi za maamuzi na ndio maana tunataka katiba yenye kututambua kama sehemu ya jamii inayopaswa kulindwa na kupata huduma za kibinadamu, " alisema Abdul.
Bw. Zungu alisema wanashangazwa na jamii kuwatenga na kuwanyima kuwapa huduma muhimu kwa tuhuma kuwa vitendo wanavyofanya havimpendezi Mungu."Tunaiomba Serikali iangalie upya kwa kuweka kifungu ambacho kitatulinda kwani kutokana na hali yetu tumekuwa tukikumbana na kero mbalimbali ikiwemo ya kutengwa na jamii, " alisema.
Mshiriki huyo alisema kuwa licha ya umoja wao kuwa na sifa mbalimbali lakini wanapofanya maombi ya kazi katika ofisi mbalimbali wamekuwa wakinyimwa bila ya sababu.
Alidai kuwa si kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi yoyote ya kuwapatia maslahi bali kinachofanyika ni kukosa nafasi hizo na kujikuta hawana kazi ya kufanya na badala yake huendeleza
ushoga ili kupata kipato cha kuwawezesha kuishi."Kama Mungu angekua hatupendi basi hata leo sisi tusingeweza kuishi hapa duniani nanyi hivyo hakuna sababu ya kututenga kuishi nanyi. Haya ni matwakwa yake," alisema.
Kwa upande wa suala la afya alisema wamekuwa wakinyanyapaliwa hasa pale wapohitaji huduma hizo na wakati mwingine huduma hizo huzipata kwa ubabe kwa baadhi ya madaktari ama kutopata kabisa.
Alisema ni vyema Serikali ikawatambua mahali walipo ili nao waweze kuchangia katika mapambano ya kuunda katiba mpya ambayo itajibu mahitaji yao.
"Kama katiba haitatutambua hakuna mtu ambaye anaweza akasimama kidete kututetea na badala yake ushoga utaendelea kila kukicha huku makundi yasiyokuwa na maadili yakiibuka ndani ya jamii," alisema.
Alisema mbali ya kundi lao ambalo linaonekana kutengwa pia kuna makundi mengi ambayo Serikali imeshindwa kuyatambua na kusema katiba nzuri ni ile inayogusa makundi yote ndani ya nchi yao.
Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya alisema njia pekee ya kujibu matatizo ya wananchi ni kupatikana kwa katiba inayotokana na matatizo ya wananchi wenyewe hivyo hakuna sababu ya kuanza kujadili idadi ya kurasa wakati matatizo hayajainishwa.
"Wakati mwingine utasikia viongozi wa Serikali wakikosoa jitihada za wanaharakati wakidai kuwa wanaleta mlolongo wa mambo mengi ni katiba gani tutakayoandika yenye kuingiza mambo yote hayo?, " alisema
Hata hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya mashoga katika tamasha hilo na kuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria ambao hawajapata kuwaona 'laivu' huku wengine baadhi ya wakiangua kilio na wengine kicheko.

Toa Maoni Yako:
0 comments: