VICHWA vipya kwenye maswala ya usanifu  ‘graphics’ na uhariri ‘editing’ kwenye  fillamu na muziki wa bongo Francis na Frank George Ntevi  ambao ni mapacha wametamba kufanya kweli kwenye anga hizo ilikuleta mabadiliko ya kweli kwenye soko la filamu na muziki wa Bongo.

Wakizungu na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, Mapacha hao walisema kua mpaka sasa wamesha  fanya kazi za kuongoza na kuihariri  filamu ya ‘The Magic Flower’ ya msanii na kiongozi wa shirikisho la wasanii  Tanzania (TAFF)Simon Mwakifamba.

“Mpaka sasa tumesha fanikiwa kuongoza filamu ya The Magic flower ni hakika itakapoingia sokoni watanzania watakubali kiwango cha filamu na utundu uliotumika kwenye filamu hiyo” walisema Mapacha hao.

Mbali na filamu hiyo pia waliweza kufanyia  graphis filamu za ‘Time after time’ iliyoigizwa na mastaa wa Bongo Izzo Bzness, Quick  Raca, Jackline  Wolper  na  filamu nyingine  ni ya  ‘My Angel’  part 1-2 ya Yusuph Mlela huku filamu zingine wanazozifanyia  graphics na editing zipo mbioni kutoka hapo baadae.

Frank na Francis ama  ‘The Squares’  wamekua wakifanya shuguli hizo za chini  ya studio ya Ntevi Pro vision ya Magomeni jijini Dar es Salaam iliyo chini ya baba yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: