Halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro imewafukuza kazi watumishi wawili wa Halmashauri hiyo akiwemo afisa mtendaji wa kijiji cha MANDE kata ya OLD MOSHI kwa kosa la wizi wa vocha 143 za pembejeo zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Tatu.

Akitoa uamuzi wa kufukuzwa kazi kwa watumishi hao katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo MORIS MAKOI amesema licha ya afisa mtendaji huyo kuiba vocha hizo pia aligushi hundi ya malipo ya shilingi laki tano na kuichukua kinyume cha taratibu na sheria kwenye akaunti ya kata.

Hatua ya kufukuzwa kazi kwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya MOSHI vijijini akiwemo Afisa mtendaji wa Kijiji cha MANDE, EMILY SUNGUSIA na dereva EDINTON KIMARO inafuatia kukamilika kwa taratibu zote za kiuchunguzi na kwamba wamefanya hivyo ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa halmashauri hiyo ambao wanakiuka taratibu za kazi.

Pamoja na kuwafukuza kazi watumishi hao, Halmashauri hiyo pia imetoa karipio kali kwa Afisa mtendaji wa kata ya Uru Kaskazini Ronald Tenga kwa kosa la utoro kazini jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Katika hatua nyingine baadhi ya madiwani wameikataa taarifa ya fedha na kuirudisha katika kamati ya fedha na mipango ili ifanyiwe marekebisho kwa madai ya kuwepo na mapungufu katika taarifa hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: