Viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakigonganisha chupa za Grand Malt katika uzinduzi wa kinywaji hicho leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi, Meneja wa Grand Malt Consolata Adam na Meneja Masoko wa kinywaji hicho, Fimbo
---
Na Mwandishi Wetu Kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kinachotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambacho kimekuwa kikipatikana katika kopo, sasa kitapatikana pia katika chupa la mililita 330.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt imezindua chupa mpya ya aina yake yenye ujazo wa mililita 330 katika kiwanda chake cha Dar es Salaam leo.
Grand Malt imekuwa ikiuzwa kwenye kopo zenye ujazo wa mililita 330 lakini kuanzia jana, itapatikana pia kwenye chupa mpya itakayouzwa sh 1000 kwa chupa na sh 20,000 kwa katoni kwa bei ya reja reja.
“Chupa hii mpya itaziba pengo katika soko na kukifanya kinywaji hiki kupatikana kwa urahisi,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja huku akisisitiza kuwa kinwaji hicho bado kitapatikana kwenye kopo pia.
Alisema Grand Malt ilizinduliwa Aprili mwaka jana lakini kwa sasa ni kinywaji namba moja kisichokuwa na kilevi Tanzania.
“Tunawashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kukikubali kinywaji hiki na kukifanya kiwe namba moja. Tunawahakikishia kuwa kitakuwepo sokoni muda wote ili kuendelea kuwaburudisha watanzania,” alisema Minja.
“Tunapozindua kinywaji hiki leo, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa kinywaji kitakachouzwa kwenye chupa ni sawa na kile ambacho kinauzwa kwenye kopo, ambacho kina vitamini na mchanganyiko wa maziwa ya aina yake,” alisema Minja.
Meneja wa Grand Malt Consolata Adam alisema, “Grand Malt ilizinduliwa Tanzania mwaka jana na leo tunapozindua chupa hii mpya, tunawashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono.”
Alisema kinywaji hicho kimetokea kuwa bora kwa sababu ya ladha yake nzuri inayoifanya inyweke kirahisi kwa kuwa ina vitamini, laktosi yenye ladha nzuri, inayoitofautisha na malt zingine sokoni.
“Kinywaji hiki kinawafaa wafanyakazi wenye shughuli nyingi lakini pia kinafaa kwa matumizi ya nyumbani, wafanyakazi wa usiku, wanafunzi, vikao vya kibiashara na sherehe nyinginezo,” alisema Consolata.
Alisema TBL itaendelea kukitangaza na kusambaza kinwaji hiki na kuhakikisha kinawafikia watanzania wengi zaidi popote walipo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: