Bi. Trinidad Jimene
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uhispania Bi. Trinidad Jimenez amesema ana mataumaini makubwa kuwa Jumuia ya nchi za Ulaya (EU) inaweza kuleta msukumo wa kuiunga mkono Palestina kuwa taifa lake, shirika la habari la Israeli, limeripoti habari hii. 

Bi. Trinidad Jimenez alisema: “Mkutano wa Septemba 2, mwaka huu wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jumuia hiyo ni jukwaa zuri la kuonesha kuuinga mkono Palestina.” 

Aliongeza kusema kuwa kuna kkila dalili kwamba wakati sasa umefika kwa kulishughulikia jambo hili haraka iwezekanavyo la Palestina kuwa huru . 

Bi Jimenez aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na gazeti la ‘El Pais’ la nchi hiyo. Wapalestina wamekuwa katika kampeni za kuitaka Umoja wa Mataifa kutamka kuwa Palestina ni nchi na inayotambulikana ikiwa na Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, pamoja na Jerusalemu iliyoporwa wakati wa vita vya siku sita vya mwaka 1967. 

Mpaka sasa hivi, nchi zaidi ya mia moja tayari zimekwisha kuidhinisha mpango wa Palestina kujitwalia uhuru wake, kwa mujibu wa azimio la mwaka 1988.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: