SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza vita rasmi kwa wale wanaovaa nguo fupi na zingine zinazofanana na nusu uchi wachukuliwe hatua kali visiwani wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
Tayari serikali hiyo imeshaiagiza Jeshi la Polisi kuachukulia hatua wale wote watakaoonekana kuvaa mavazi hayo
Tamko hilo limetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kujitokeza kwa baadhi ya watu kuonekana wakila chakula hadharani nyakati za mchana
Mbali na hilo pia amesema baadhi ya wanawake wamekuwa wakionekana mitaani wakiwa wamevaa nguo fupi na zingine zisizokuwa na heshima kabisa na kuonekna kwa baadhi ya vijana wakiwa wamelewa chakari mchana wa Ramadhani.
Nyumba za kulala wageni na migahawa imeonekana kutoa huduma mchana kipindi cha mfungo kwanikufanya hivyo ni kinyume cha sheria pamoja na kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mafundisho yake Mtume Mohammad,” alisema.
Waziri huyo amesema maamuzi yamekuja ili kuweza kurudisha hadhi ya kipindi cha nyuma visiwani humo wakati wa mwezi wa Ramadhani kumekuwa hakutendeki mambo hayo kama ilivyo sasa.

Toa Maoni Yako:
0 comments: