Balozi wa Palestina huko Umoja wa Mataifa Bwana Riyad Mansour amesema jana Jumatano kuwa Israeli inasisitiza msimamo wake wa kupanua makazi ya walowezi katika ardhi inayoikalia badala ya kufanya juhudi za kutafuta amani ya kweli ambayo itamaliza kabisa ukaliwaji wa kimabavu unaofanywa na Israeli katika ardhi ya Palestina tangu Juni mwaka 1967.

Haya kayasema katika barua aliyompelekea katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia raisi wa Baraza la Usalama la umoja huo.

Amesema katika matamshi ya sasa hivi ya Israeli kuwa ina mpango wa kujenga nyumba mpya zipatazo 2500 huko Jerusalem ya Mashariki.

Serikali ya Israeli ilitangaza tarehe 15 Agosti kuwa iko mbioni kujenga nyumba mpya 277 huko 'Ariel' katika Ukingo wa Magharibi.

Anasema kwa tangazo hilo la hivi karibuni Israeli imesema itajenga makazi 2800 katika kipindi kisicho zidi wiki mbili.

Alisisitiza kuwa kuna makubaliano kote duniani kuwa mpango huu wa Israeli ni kinyume na sheria za kimataifa na kwamba hauruhusiwi, ni batili kufanyika.

Alisema kuwa kushindwa kwa jumuia ya kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama kuikemea Israeli kusitisha mpango wake huo; kunaihalalishia serikali hiyo dhalimu ya Israeli kuendelea na ubabe wake wa kupanua makazi ya walowezi wa kiyahudi kwa kuwanyang’anya Wapalestina ardhi yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: