Mmoja wa wasimamizi wa watoto wa kituo hicho akisaidia kugawa maji kwa watoto hao walioonekana kuchangamka kupita kiasi.
Mmoja wa wasimamizi wa watoto wa kituo hicho akisaidia kugawa futari kwa watoto hao walioonekana kuchangamka kupita kiasi.
Pichani kulia ni Mwanaharakati na muelimishaji wa masuala mbalimbali ya Kijamii yakiwemo ya watoto, Mama Sadaka Gandi akishirikiana na Kampuni ya Prime Time Promotions wakijumuika pamoja na watoto wa kituo cha kulelea  watoto yatima wapatao 75 kiitwacho Mwana Orphan Center,kilichpo Vingunguti jijini Dar jioni ya leo kwa ajili ya futari walioiandaa maalum kwa watoto hao.
Watoto wakifuturi kwa umoja na mshikamano.
Watoto wa kituo cha Mwana Orphan Center wakipata futari pamoja jioni ya leo.Aidha kituo hicho kina jumla ya watoto wapatao 75 ( wa kike 35 na kiume 40).Blog ya Jiachie pia ilialikwa kwenye futari hiyo jioni ya leo,lakini pia ilibahatika  kuzungumza na mlezi wa kituo hicho aitwaye Dada Umi,alisema kuwa kituo hicho kinahitaji msaada mkubwa wa vitu mbalimbali vya shule yakiwemo,madaftari,pia aliongeza kuwa wanahitaji Magodoro kwani waliyonayo yamekwisha chakaa,Vyakula pamoja na msaada wa huduma ya matibabu kwa namna moja ama nyingine..

"Kikubwa zaidi tunaomba msaada wa tupatiwe jenerata kwa ajili ya kusukumia maji kwenye matanki yetu tunayohifadhia maji,ambao ndio mradi wetu mkubwa tunaoutegemea,unaotuingizia fedha kiasi kwa ajili ya kujikimu,kwa sababu maji hayo tunawauzia watu wanaotuzunguka kwenye kituo hiki,ambao ni wengi sana",alisema Dada Umi ambaye amedumu kwenye kituo hicho kwa muda wa miaka nane mpaka sasa.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: