Jenerali Slyvester Rioba.
Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), limesema watumishi pamoja na wananchi wengi nchini hawana elimu ya kutosha kuhusiana na matumizi ya huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya mikopo.

Akifungua semina juu ya elimu ya ujasiriamali na uwekezaji kwa wanajeshi, Mkuu wa operesheni na mafunzo JWTZ, Jenerali SLYVESTER RIOBA, alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wananchi wanakopa fedha na huzitumia katika shughuli za kijamii badala ya kuzitumia katika uzalishaji na uwekezaji.

Aidha amesema watatoa mikopo kwa watumishi wa JWTZ, pamoja na wafanyakazi wengine wa wizara ya ulinzi nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwawezesha kupambana na umaskini na kukuza uchumi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: