Mcheza filamu ‘hot cake’ Bongo, Wema Abraham Sepetu, hivi karibuni amewafurahisha mashabiki wake baada ya kueleza kuwa, amepima Virusi vya Ukimwi (VVU) mara tu aliporejea kutoka Marekani na kubaini kuwa, eti hana virusi.Wema ambaye huko nyuma amewahi ‘kutoka’ na mastaa mbalimbali (pichani ukurasa wa mbele) kabla ya kudondokea kwa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa katika Kipindi cha Mkali wa Afro cha Redio Times FM.

Akizungumza kwa mbwembe, Wema alisema alichukua uamuzi huo baada ya kupendana kwa dhati na Diamond hivyo akaona ili wayafurahie maisha yao ni vyema akapime.“Niliporudi kutoka Marekani, tulikwenda kupima, mimi na ‘baby’ wangu mara tatu na tukakutwa salama kabisa hivyo tunajiamini na tunafanya mapenzi yaliyo salama bila kutumia kondom.

“Hivi sasa natamani sana mtoto na kwa sababu nimepima sina tatizo lolote, nikipata ujauzito siwezi kutoa, nitazaa kwa vile na baby anataka mtoto, hakuna tatizo,” alisema Wema.

Aidha, msanii huyo ambaye amekuwa akikumbwa na misala ya kupelekwa polisi kila mara aliongeza kuwa, ni bora azae mapema ili hata atakapokufa awe ameacha ‘chata’ yake.

“Nimepanga kuzaa kwa sababu lazima niache chata yangu maana unaweza kufa hujaacha kumbukumbu yoyote. Napenda sana mtoto wa kike lakini mwenzangu anapendelea sana mtoto wa kiume,” alihitimisha Wema.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. wemA NI KICHECHE ALIESHInDIKANA ..........NA NGWENGWE ANAYO >..LABDSA ALIPIMA VIRUSI KWA WACHINA KUDADADEKI..>>>

    ReplyDelete