Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa (UN) amesema “amesikitishwa sana” na vurugu zilizotokea katika Milima ya Golan, ikipelekea watu kama 40 kuuawa.
"Kati ya waandamanaji 30 hadi 40 inasemekana wameuliwa na majeshi ya Israeli katika muda wa wiki tatu zilizopita," alisema Bi Navi Pillay katika taarifa yake ya Jumanne.
"Serikali ya Israel inawajibu wa kuhakikisha kuwa majeshi yake hayatumii silaha au nguvu za ziada," alisisitiza Bi Pillay ambaye ni kamishna wa haki za binadamu katika UN.
"Hata kama mazingira yakiwa magumu, utumiaji wa risasi za moto kuwashambulia waandamanaji wasio na silaha, inasababisha raia wasio na hatia kufa au kujeruhiwa kwa wingi, na jambo hili linazusha maswali mengi kuhusu utumiaji wa silaha"
Majeshi ya Israeli yalitumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji waliokuwa karibu na milima ya Golan kwenye mipaka ya Syria siku ya Jumapili.
Waandamanaji hao walikuwa wakidai Israel ikomeshe uvamizi wake wa maeneo ya Golan.

Toa Maoni Yako:
0 comments: