Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Lucy Nkya (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari sindano zinazoruhusu kutumika mara moja kwa mgonjwa na kuepusha matumizi zaidi ambayo wakati mwingine hayazingatii usafi hivyo kusababisha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Msaada wa Sindano hizo umetolewa leo na Shirika la Safe Point utasambazwa katika hospitali za mikoa ya Lindi, Morogoro na Mwanza.

Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Lucy Nkya (katikati) akipokea msaada wa maboksi yenye sindano kutoka kwa Bw. Marc Koska(wa pili kutoka kulia) mwasisi wa Taasisi ya kujitolea ya Safe Point Trust ya Uingereza ikiwa ni ishara ya kupokea msaada wa kontena 1 lenye sindano zenye viwango vya kimataifa ambazo huruhusu kutumika mara moja kwa mgonjwa mmoja na hivyo kupunguza maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia ni Mganga mkuu wa Serikali Dkt Deo Mutasiwa (kushoto) na Dkt. Magreth Muhando (kulia).Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Lucy Nkya akizungumza na waandishi wa habari na wataalam wa Afya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kabla ya kupokea msaada wa kontena lenye sindano kwa matumizi salama zenye viwango vya kimataifa ambazo huruhusu kutumika mara moja kwa mgonjwa mmoja na hivyo kupunguza maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi kutoka Taasisi ya kujitolea ya Safe Point Trust ya Uingereza leo jijini Dar es salaam.Mwasisi wa Shirika la Safe Point ambayo ni taasisi ya kujitolea yenye makao yake nchini Uingereza Bw. Marc Koska akiwasilisha mada kwa viongozi, wataalam wa Afya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni mbalimbali za njia salama ya matumizi ya sindano na namna shirika hilo linavyofanya kazi leo jijini Dar es salaam.

Mwandishi wa habari na mpiga picha wa kituo cha Televisheni cha Chanel 10 Bw. Kibwa Dachi (katikati) akipata maelezo ya namna moja ya video kamera inayotumiwa na watalam wa picha kutoka kampuni ya kutengeneza filamu ya Hollywood ya Marekani inavyofanya kazi leo jijini Dar es salaam. Watalam hao kutoka Hollywood ni miongoni mwa wageni walioambatana na Shirika la Safe Point la nchini Uingereza kutoa msaada wa kontena la Sindano zenye viwango vya kimataifa vya Life Saver kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: