Hapa ni kazi tu, vijana wakionyesha umahili wao wa kuigiza.Hapa mzuka ulikuwa umepada zaidi.Hawa ndiyo majaji wa Serengeti Fiesta Filamu inayoendelea ndani ya viwanja wa Leaders Clubn jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni shoto ni mtangazaji wa Clouds Tv katika kipindi cha Take One ambaye pia ni mratibu wa Serengeti Fiesta Filamu, muigizaji Shamsa Ford, Yusuph Mlela, pamoja na Simple ambaye ni muigizaji wa tamthilia iitwayo 69 Record.

Hawa ni vijana waliojitokeza katika mchakato wa kutafuta mkali wa Serengeti Fiesta Filamu.Take one, action ndiyo waliyouwa wakisubiri.

Majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Filamu 2011 iliyofanyika ndani ya viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Simple ambaye ni muigizaji wa tamthilia iitwayo 69 Record, muigizaji Yusuph Mlela, Shamsa Ford, mtangazaji wa Clouds Tv katika kipindi cha Take One ambaye pia ni mratibu wa Serengeti Fiesta Filamu pamoja na muongozaji wa filamu William Mtitu.Mwendesha mitambo kutoka Clouds Tv aitwaye Razack Ford akiweka mambo sawa.Mtangazaji wa Clouds Fm Wasi wasi Mwabulambo (kushoto) ambaye pia alikuwa ni muongozaji wa zoezi hilo akitoa maelezo kwa washiriki waliojitokeza.

Hawa ni vijana waliojitokeza katika mchakato wa kutafuta mkali wa Serengeti Fiesta Filamu.

Ni Serengeti Fiesta Filamu iliyofanyika ndani ya viwanja vya Leaders Club ambapo vijana wamepata mwamko wa kutoka na jumla ya vijana wapatao 1200 wamejitikeza katika zoezi hilo la usaili wa Serengeti Fiesta Filamu. Machakato huo wa kumtafuta mkali wa kuigiza ulianza mapema kabisa leo majira ya saa nne asubuhi na zoezi hilo halikuisha linatarajiwa kuendelea kesho. Inaonyesha kuwa watu wengi hasa vijana wa jijini Dar es Salaam wanapenda sana kuwa wasanii wa filamu ndiyo maana wamekuwa na mwamko.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: