Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwepo kwa Vyama Vingi vya Siasa nchini siyo kuleta uadui bali ni kupanua demokrasia na kuleta utawala bora ili kupata maendeleo ya haraka.
Mhe. Pinda alikuwa akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa wanaounda Baraza la Vyama vya Siasa (Council of Political Parties) nchini, katika hafla aliyowaandalia kwenye makazi yake mjini Dodoma jana (Jumatano Juni 8, 2011) usiku.
Alisema kwa mantiki hiyo ndiyo maana Bungeni, pamoja na hoja kali lakini Wabunge wa Vyama mbalimbali siyo maadui. “Tunafanya kazi pamoja, tunakula pamoja, tunacheka pamoja na wakati mwingine utafikiri wote tunatoka Chama kimoja”.
Aliwaelezea wajumbe hao hatua mbazo Serikali inachukua katika mchakato wa Katiba mpya na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/12 iliyowasilishwa Bungeni mjini Dodoma jana (Jumatano Juni 8, 2011).
Waziri Mkuu alisema pia Serikali itaziangalia na kuzifanyia kazi hoja za Baraza za kutaka liwezeshwe, litangazwe kwa wananchi ili walitambue vizuri na lipewe nafasi kubwa ya kuishauri Serikali katika masula ya kitaifa na ya kisiasa.
Hoja hizo zilitolewa na baadhi ya Wajumbe waliopata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo.
Wajumbe walimshukuru Waziri Mkuu kwa kukutana nao kama Baraza. Vilevile walikiri kuwa ni mara ya kwanza kwa Kiongozi wa kitaifa wa ngazi yake kukutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa vilivyosajiliwa na kubadilishana mawazo kwa uhuru.
Walitaka mawasiliano baina ya Serikali na Baraza yaendelezwe kwa manufaa ya taifa.
Baraza hilo limeundwa kisheria kwa marekebisho ya mwaka 2009 ya Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992. Kazi yake kubwa ikiwa kuishauri Serikali katika mambo ya kitaifa na yanayovihusu Vyama vya Siasa, hasa katika kutatua migogoro ya Vyama hivyo kila inapozuka.
Linaundwa na Vyama 18 vya Siasa vilivyopata usajili wa kudumu, kutoka pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano, na Sekretarieti yake iko chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa pia alikuwepo katika hafla hiyo na aliahidi kuwa Ofisi yake itajitahidi kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli za Baraza hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments: