Pamoja na wilaya ya Makete kuwa ni wilaya inayoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI vita na mapambano dhidi maambukizi hayo huenda isifanikiwe ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa. Hii ni kutokana na milango ya kituo cha uchauri nasaha na kupimia VVU cha hospitali ya Bulongwa kufungwa kwa takribani wiki mbili sasa.
Katika hali isiyo ya kawaida hospitali kubwa ya misheni Bulongwa imefunga milango ya kituo cha ushauri nasahaa na upimaji wa VVU kutokana na kuishiwa vitendanishi vya kupimia virusi vya UKIMWI. Hospitali ya Bulongwa inayomilikiwa na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya kusini kati inahudumia eneo lenye wakazi zaidi 30,000.
Vitendanishi vya D-Bioline na Determine vinavyotumika kupima iwapo mtu ana maambukizi ya VVU hutolewa bure na ofisi ya mganga mkuu wa wilaya. Toka wiki iliyopita watu kadhaa wenye mahitaji ya kupima virusi vya UKIMWI walikosa huduma hiyo baada ya kufika katika kituo ushauri nasaha na upimaji wa VVU cha hospitali ya misheni Bulongwa na kurudi bila kupima baada ya kuambiwa hawawezi kupimwa kutokana na kukosekana kwa vitendanishi hivyo.
Miongoni mwa watu wengi waliokosa huduma hiyo wametembea umbali mrefu kutoka vijiji vya mbali kama Unyangala (kilomita 40) na Uganga (kilomita 50). Upimaji wa virusi vya UKIMWI kwa hiari ni njia mojawapo ya kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI. Kampeni za upimaji kwa hiari wa nchi nzima zilizinduliwa na mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2007 kwa kauli mbiu ya Tanzania Bila UKIMWI inawezekana.
Kiwango cha maambukizi kwa sasa katika wilaya ya Makete ni 16.9% ukilinganisha na kiwango cha kitaifa cha 5.7% mkoa wa iringa una wastani wa maambukizi wa 13.4%.
Wanaharakati wa haki za binadamu na watu wanaoishi na VVU wanaulaumu uongozi wa hospitali ya misheni ya Bulongwa kwa Uzembe wa makusudi na kushindwa kutimiza wajibu wake. Hii imesababisha adha kwa wateja wake na hata kukwamisha mapambano dhidi ya UKIMWI. “Hii sio mara ya kwanza hospitali hii kuishiwa aidha dawa au vitendanishi. Miezi miwili iliyopita hospitali ilikuwa imeishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU za ARV na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa huduma hiyo’’.
Mara kwa mara huduma za tiba zinazopaswa kutolewa bure huwa zinakuwa na matatizo ya kuishiwa aidha dawa au vitendanishi, watumiaji wa dawa za TB mathalani wamekuwa wakikosa huduma kufuatia kuisha kwa dawa ghalani. Huduma za uzaz, mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 7 bado zinalipiwa tena kwa bei kubwa, ingawa mwongozo wa serikali unataka huduma hizo zitolewe bure. Watu wanaoishina VVU wamekuwa hawapimwi kinga zao kwa kama mwongozo wa shirika la afya duniani na wizara ya afya vinavyotaka
Hospitali zinatakiwa kuagiza dawa MSD, wasambazaji dawa miezi mitatu kabla kwa ajili ya kupata dawa hizo mapema.” Sasa kama mpaka leo tayari kuna upungufu wa vitendanishi ili hali MSD ilikuwa wazi hali itakuwaje kwa mwezi wa sita na wa saba kufuatia kufungwa kwa MSD mwezi wa sita kwa kupisha stock taking?”

Toa Maoni Yako:
0 comments: