JERUSALEM – Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Uislamu Dk. Ekrima Sabri amesema kuwa baada ya miaka ishirini na mitano ya kufukua, watafiti wa mambo ya kale (wanaakiolojia) wametamka kuwa hakuna chembe ya ushahidi wala jiwe linaloonesha kuwa mji wa Jerusalem uliwahi kukaliwa na Mayahudi na kwamba historia yao haipo kabisa katika mji huo.
Sheikh Sabri alisema juhudi za Israeli kufungua Uwanja wa Kibliakusini mwa msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa ulioko mashariki mwa Jerusalem ni njama tu ya kufuta alama za kihistoria za kiislamu.
Mamlaka ya Israeli imekuwa ikijenga Bustani ya Kibiblia juu ya hekalu la Umayyad huko Jerusalem. Lakini Bwana Sabri amesema kwamba wanaikolojia wamekubaliana kwamba mawe yanayopatikana huko ni ya enzi za utawala wa Umayyad.
“Kamwe hatukubali alama za kiislamu zifutwe na urithi wetu upotee, muda wote wa uhai wetu, bila shaka tutafaulu katika suala hili,” alisema Bwana Sabri. Shirika la Kimataifa la nchi za Kiislamu (OIC) tayari limeshutumu vikali hatua ya Israeli ya kufungua Bustani ya Kibiblia karibu na msikiti wa Al-Aqsa.

Toa Maoni Yako:
0 comments: