Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Jacksom Mmbando akimkabidhi dawati la majani (lapdesk) kwa diwani wa kata ya Segerea Azuri Mwambagi (katikati) kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Misewe ya jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rotary Club North ya Dar es Salaam Massimo Tognetti ambao pia walishirikiana na Tigo kutoa msaad huo. Jumla ya madwati 1000 na viti 1000 vilikabidhiwa jana shuleni hapo.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando akiwa na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Misewe ya Ilala jijini Dar es Salaam mara baada ya kampuni hiyo kwa kushirikian na Club ya Rotary North ya Dar es Salaam kukabidhi madawati 1000 ya mapajani (lapdesks) na viti 1000 kwa shule hiyo.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya Msingi ya Misewe jinsi ya kutumia madawati ya mapajani (lapdeks) mara ya kukabidi madawati hayo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Mei 31, 2011, Dar es Salaam. Katika jitihada zake za kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Club ya Rotary North ya jijini Dar es Salaam imetoa msaada wa viti 1000 na madawati 1000 katika shule ya Msingi ya Misewe ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Tigo na Rotary Club North wamefikia umamuzi wa kutoa msaada huo kwa kuthamini umuhimu wa elimu ya shule ya msingi. Halikadhalika kwa kuzingatia kuwa watoto wa leo ndiyo watakuwa viongozi wa kesho kwahiyo ni vyema kuwaboreshea mazingira ya elimu.

Afisa uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando alisema “ Tunajisikia furaha sana kuwasaidia watoto hawa ambao ni viongozi wa kesho ili kupunguza tatizo lao la kukaa chini wakati wakiwa madarasani wakipata elimu yao ya kila siku.

Alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo hasa ni kusaidia badhi ya shule za msingi ambazo zimekuwa na hukosefu wa madawati na kuongezea kuwa msaada huo utaendela kutolewa katika shule nyingine za msingi zenye uhaba wa madawati.

Akiongea katika utaoji wa madawati, diwani wa Segerea bw Azuri Mwambagi alishukuru sana kwa msaada wa madawati yamapajani ikitoka kampuni ya simu ya mkononi Tigo na viti vikitoka Rotary International. Aliongezea kwamba makampuni mengine yafanye wanavyofanya Tigo na Rotary International na kwa sasa wanahitaji madawati 18,000 na siyo jukumu ya serikali tu lakini yawatanzania kusaidia watanzania wenzao.

Naye akiongea kwa niaba wa Rotary, gavana msaidizi bw Massimo Tognetti alisisitiza haja yakuendeleza elimu Tanzania. Rotary International ni taasisi yakimataifa na zaidi ya wanachama million 1.2 na mbinu zake za msingi ni “kufanya mema katika dunia hii” ikiwafaniskisha warotaria katika ulimwengu kuelewa, kuwa na moyo, ukarimu, na amani kwa njia ya afya njema, msaada wa elimu na kupunguza umaskini. Hii ni hatua nyingine kuelekea katika malengo ya Rotary ikiboresha elimu na kuandika nchini Tanzania na tumefurahi kushirikiana na Tigo katika kutimiza malengo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: