Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa miongoni mwa maelfu ya wakazi wa mjini Dar Es Salaam waliomzika Mnajimu Mkuu wa Tanzania, Sheikh Yahya Hussein, Jumamosi, Mei 21, 2011, kwenye Makaburi ya Tambaza mjini Dar es Salaam.

Rais Kikwete amewasili kwenye Makaburi ya Tambaza muda mfupi tu baada ya kurejea nchini akitokea Namibia ambako jana, Ijumaa, Mei 20, 2011, alishiriki katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Kikwete ameshiriki kuupokea mwili wa Sheikh Yahya Hussein uliofikishwa makaburini kiasi cha saa 10.50 adhuhuri ambako mazishi yalianza dakika tano baadaye.

Sheikh Yahya Hussein ambaye katika maisha yake alijipatia umaarufu ndani ya jamii kwa kipaji chake cha unajimu, alifariki dunia asubuhi ya jana, Mei 20, 2011, akiwa anakimbizwa kupelekwa hospitali. Sheikh Yahya aliyekuwa na umri wa miaka 80 alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: