WAZIRI mkuu wa Israeli Bwana Benjamin Netanyahu aliliambia Baraza la Congress la Marekani kuwa atayaondoa makazi ya walowezi ikiwa tu kutakuwa na makubaliano ya kweli ya amani na Wapalestina.

Lakini akakataa katakata matakwa ya jumuia ya kimataifa yanayoitaka nchi hiyo kurejesha ardhi iliyoikwapua hadi kufikia mipaka ya mwaka 1967 au kuugawana mji wa Jerusalem.

Netanyahu pia alikataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati yake na Rais wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas huku kukiwa na Chama cha Hamas.

Akaongeza kusema kuwa jambo ambalo linakwamisha kufikiwa kwa amani ya kudumu ya mzozo huo ni kukataa kwa Wapalestina kuitambua Israeli.


"Tutakuwa wema juu ya ukubwa wa taifa la Palestina," alisema huku akishangiliwa na wajumbe wa Baraza hilo.

Wapalestina kwa upande wao wanataka Jerusalemu ya Mashariki iwe mji wao mkuu wa taifa jipya la Palestina.

"Kwa kusema ukweli Jerusalem haiwezi kugawanywa tena. Jerusalem inabaki mji mkuu wa taifa la Israeli," Netanyahu alisema.

Obama, wiki iliyopita alisema Marekani na Jumuia ya Kimataifa wanataka taifa la Palestina liundwe kulingana na mipaka ya iliyokuwepo kabla ya vita ya siku sita ya mwaka 1967.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: