Nashukuru sana wale wote ambao tumeshirikiana kwa wakati wote nikiwa afisa habari wa Simba Sports Club,nashukuru pia hata kwa wale ambao hawakuonesha ushirikiano kwangu na kwa wale wote wanaonichukia,kuanzia May 11 nimeacha kazi ya uafisa habari wa Simba. Hayo ni maneno ya Cliford Mario Ndimbo kutoka katika ukurasa wake wa facebook.
------
Baada ya kuitumikia klabu ya Simba Sports kwa takribani mwaka mmoja na nusu,kwa matakwa yangu binafsi pasipo kushawishiwa na mtu yeyote nimeamua kuacha kazi.
Sababu kubwa iliyonipelekea kuacha kazi ya Uafisa habari wa Simba, pamoja na mambo mengine lakini nimeona kuna mambo kadhaa ambayo hatuendi sawa kiasi cha kuweka ugumu kwenye kazi yangu (kutozingatiwa kwa uweledi yaani professionalism)
Nashukuru kuwa nilifanya kazi nzuri wakati wa uongozi uliopita chini ya mwenyekiti Jemedari Hassan Dalali iliyopelekea uongozi wa sasa chini ya Alhaj Ismail Aden Rage kuhitaji kuendelea kupata huduma yangu.
Kwa kipindi chote ambacho nimekaa na uongozi uliopo madarakani nimekuwa nikitekeleza majukumu yangu japo wakati mwingine katika ugumu ambao nilipohoji niliambiwa yote yatatatuliwa.
Hii inakuwa barua yangu ya pili kuandika kuhusu kuacha kazi baada ya ile ya awali April 5 2011 kutokubalika baada ya kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na katibu mkuu na kushauriana mambo kadhaa ambayo yalinirudisha kuendelea kuitumikia Simba Sports lakini nimeamua kuacha kazi baada ya kuona hata yale niliyoahidiwa yatashughulikiwa yakiwa bado yapo vilevile japo tulizungumza kwa pamoja na wajumbe wa kamati ya fedha na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji kwenye kikao tulichokaa Jumatatu March 28 2011 makao makuu ya klabu kuanzia saa 7 mchana.
Nashukuru kwa ushirikiano ambao nimepata kutoka kwa wanachama,wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Simba kwa kipindi chote ambacho nimetumikia, nashukuru nimeamua kuondoka kwa amani na naamini atapatikana mtu mwingine makini katika nafasi hiyo ambaye ataendelea pale nilipoacha.
Kwangu ni experience kubwa nimeipata katika soka la Tanzania na vilabu kupitia Simba Sports Club ambayo naamini ni somo kubwa kwangu.
Mwisho nawatakia kila la kheri katika harakati za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la Simba Sports na nawatakia Amani.
CLIFORD MARIO NDIMBO

Toa Maoni Yako:
0 comments: