Na Mwandishi wetu

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu cha Ardhi vimepata ushindi katika mchezo wa soka katika tamasha la promosheni ya Excel with Grand Malt lililofanyika juzi katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Da es Salaam.

IFM walipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Chuo Cha Ustawi wa jamii, halikadhalika Ardhi walijishindia magoli 2-0 dhidi ya Chuo Cha Biashara (CBE). Magoli ya IFM yalifungwa na Mfuta Ngonyani na Yusufu Khamis. Kwa upande wa Ardhi magoli yote mawili yalifungwa Pirmin Mzenga.

Vyuo vyote vilivyoshiriki katika bonanza hilo vilivyojinyakulia zawadi mbalimbali yakiwemo mabegi ya kisasa ya kubebea vitabu pamoja na fulana za Grand Malt.

Akiongea katika bonanza hilo, mwakilishi wa Mauzo wa TBL kanda malum ya Dar es Salaam, Flavian Ngole alisema kuwa wamefurahishwa na jinsi wanavyuo wa vyuo vya elimu ya juu vya Dar es Salaam vilivyopokea wito wa kushiriki katika bonanza hilo.

“Ningependa kuwashukuru wanavyuo kwa witikio wenu mzuri katika tamash hili la promosheni ya Execl With Grand Malt ambayo inawahusu nyie hasa, nina matumaini kuwa mwisho wa siku tutafikia malengo yetu, alisema Ngole.

Excel with Grand Malt ni promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake ambacho hakina kilevi cha Grand Malt, yenye lengo la kutoa tuzo za aina mbalimbali kwa wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

Washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ambapo zawadi kubwa itakuwa hundi ya kununulia vitabu yenye thamani ya shilingi laki nne. Tuzo hizo zinashindaniwa katika makundi manne ambayo ni utamaduni na burudani, huduma za jamii na mazingira, ugunduzi na kipaji maalum.

Vyuo vinavyoshiriki katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo ni Chuo cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara, Taasisi ya Jamii.

Vingine ni Chuo Kikuu Cha Elimu ya Elimu (DUCE), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa na Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: