Naibu Waziri wa Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Issa Haji Ussi, Jumatano Mei 11, 2011 atakuwa Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Mpango wa Miaka kumi ya Usalama barabarani itakayofanyika katika Viwanja vya Malindi mjini Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa Lengo kuu la Tamasha hilo ni kutaka kuimarisha masuala ya Usalama barabarani miongoni mwa vijana na kukumbusha wajibu wa kila mmoja kujitolea ili kuleta mabadiliko yatakayosaidia kupunguza ajali na kuifanya Barabara kuwa sehemu salama kwa watumia wote.

Inspekta Mhina amesema kuwa Tamasha hilo pia litahudhuliwa na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya hapa nchini (EU) Bw. Tim Clarke, hasa ikizingatiwa kuwa siku hiyo pia inakwenda sambamba na Sherehe za Umoja wa nchi za Ulaya.

Naye Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda ya Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Makame Ali Makame, amesema Sherehe hizo zitatanguliwa na Maandamano ya wanafunzi wa Shule za Msingi yatakayoanzia Shule ya sekondari Lumumba kupitia Barabara ya Malawi dahi katika Viwanja vya Michezo vya Malindi mjini humo.

Kamanda Makame amesema tamasha hilo limewalenga wanafunzi zaidi hasa ikizingatiwa kuwa watoto ni wahanga wakubwa wa matuki ya ajali za barabarani Duniani kote.

Amesema utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 1.2 Duniani wakiwemo watoto wa shule hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani na wengine milioni 50 hujeruhiwa na kubakia na vilema vya kudumu.

Kauli mbiu ni Tamasha hilo ni Jitolee kuleta mabadiliko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: