Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige (Kulia) akikabidhi pesa taslimu sh. 500,000/- kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake katika mashindano ya riadha ya mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni, Mary Naali. Mbio hizo za Kilometa 21 zilifanyika Wilayani Karatu jana zikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige (mwenye kofia katikati) akimkabidhi zawadi ya pesa taslimu shilingi laki tano pamoja na medali ya dhahabu mshindi wa mbio za TIGO Ngongoro Marathoni kwa upande wa wanaume, Fabian Joseph mjini Karatu jana. Kulia anayepiga makofi ni Meneja mauzo wa TIGO Mkoa wa Arusha, Joseph James. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria
Meneja Mauzo wa TIGO mkoa wa Arusha Joseph James kulia akikabidhi zawadi wa pesa taslimu 100,000/- kwa mshindi wa mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni Cecilia Safary zilizofanyika Wilayani Karatu jana. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria
Mwanariadha Ally Athumani akishiriki katika mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni zilizofanyika jana Wilayani Karatu chini ya udhamini wa Kampuni ya Simu za mkononi ya TIGO. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria
Wanariadha wakishiriki katika mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni zilizofanyika jana Wilayani Karatu chini ya udhamini wa Kampuni ya Simu za mkononi ya TIGO. Mbio hizo ambazo zilifanyika kwa mara ya nne mfululizo zilikuwa na lengo la kuhamasisha jamii ili kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige (wa pili kulia) wakati akizindua mashindano ya mbio za TIGO Ngorongoro Marathoni Wilayani Karatu jana. Wengine kushoto ni Asaf Simantov wa TIGO, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mathew Sondoweko na Zainab Ansell wa Zara Tours mwenye nguo nyekundu. Kulia kabisa ni Mkuu wa Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro Benard Mrunya. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Toa Maoni Yako:
0 comments: