Rais Jakaya Kikwete (kati) Balozi wa Japan nchini Hiroshi Kanagawa (kulia) wakikata utepe na Waziri wa Ujenzi John Mgufuli akizindua sherehe za kuweka jiwe la msingi katika ujenzi na upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo sehemu ya Mwenge – Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 iliyofanyika kwenye eneo la Ngome Saccos- Mwenge jijini Dares Salaam.
Waziri w a Ujenzi John Magufuli (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Rais Kikwete wakati wa sherehe hiyo.
Waziri John Magufuli (shoto na Balozi wa Japan Nchini Hiroshi Kanagawa wakiwapungia mikono wananchi katika sherehe hiyo.
Baadhi ya Maafisa ya Japan na Tanzania wakifuatilia sherehe hiyo. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa na Habari na Magreth Kinabo).
---
RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha inakubali kukabidhiwa barabara zilizojengwa katika kiwango kinachotakiwa kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa barabara hizo.

Kauli hiyo iliitoa leo na Rais Kikwete wakati wa sherehe za kuweka jiwe la msingi katika ujenzi na upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo sehemu ya Mwenge – Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 iliyofanyika kwenye eneo la Ngome Saccos- Mwenge jijini Dares Salaam.

“Hakuna sababu ya kumlipa mkandarasi wa barabara ambayo haijafikia kiwango kinachotakiwa. Waziri hili lazima liishe msiliache likaendelea mna uwezo wa kukataa kupokea mkatoa maelezo ikarekebishwa,” alisema Rais Kikwete.

Aidha Rais Kikwete aliwataka watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha barabara zinazojenga zinalingana thamani ya fedha iliyotolewa.

Rais Kikwete alisema ujenzi wa barabara hiyo umetokana na ziara yake aliyoifanya nchini Japan mwaka 2007. Aliongeza kuwa anaishukuru serikali ya Japan na wananchi kupitia balozi wa Japan kwa misaada wanayoitoa.

Aliongeza kuwa serikali itaendelea na mkakati wa kuboresha miundombinu nchini na suala la ujenzi wa barabara ni sehemu mojawapo ya miundombunu itakayoboreshwa, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 serikali imetoa Sh. Trilioi 1.3 ikilinganishwa na mwaka 2005/06 ilipotenga Sh. bilioni 470 kwa ajili ya kazi hiyo.

Kwa upande Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli alisema fedha za ujenzi wa barabara hiyo , inayojengwa na mkandasi kutoka kampuni ya Konoike ni sh. bilioni 88 zitatolewa kwa msaada wa serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA). Hata hivyo imeshatoa Sh.bilioni moja kwa jili ya usanifu.

Alisema barabara hiyo itakuwa na njia nne, mbili kila upande, njia ya waendao kwa miguu pande zote za barabara, madaraja matatu, makalvati 28 na katikati kutakuwa na barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kwa mwendo kasi (BRT).

“Ni dhahiri kuwa upanuzi wa barabara hii utapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano uliopo wa magari,” alisema Waziri Magufuli.

Magufuli alisema baada ya ujenzi huo kukamilika mwezi Mei mwaka 2013,wakati ujenzi wa barabara ya New Bagamoyo eneo la Morocco – Mwenge utaanza baada ya kukamilika kwa uhamishaji wa mali na miundo mbinu iliyopo katika hifadhi ya barabara.

Wakati huohuo, Waziri Magufuli aliwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara barabarani eneo la Tegeta kuanza kuondoka kuanzia leo (jana) na kuzingatia Sheria ya Barabara namba 13 ya mwaka 2007.

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini , Hiroshi Nakagawa alisema serikali ya nchi yake itaendelea kutoa misaada kwa nchi za Afrika kama ilivoahidi kwenye mpango wake wa kuzisaidia nchi za Afrika licha ya kuwepo tatizo la Tsunami na tetemeko la ardhi.

Alisema ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kupunguza gharama za usafiri na kukuza uchumi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: