TAREHE YA KUZALIWA: 08/08/1990
MAHALI ALIPOZALIWA: Morogoro.
1998-2004 elimu ya msingi Kinondoni shule ya msingi.
2005-2007 elimu ya sekondari aliishia kidato cha tatu.
ALBAMU YAKE;
Albamu yake ya kwanza aliifanya kwa kipindi cha kati ya 2008-2010 kwa ushirikiano na Amini iliyotambulika kwa jina la Njia Panda ambayo ilikuwa na jumla ya nyimbo 14 ambapo baadhi ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo ni pamoja na:
Muongo’ ,Robo saa, na Mbala mwezi zote zimeimbwa na Amini pamoja na Barnabas.
Wrong Number, iliyoimbwa na Barnabas pamoja na Linah
MAISHA YAKE KABLA YA MUZIKI
Baada ya kukatiza elimu yake ya sekondari alikuwa akitumia muda wake mwingi kuuza genge la vyakula lililokuwa nyumbani kwao pamoja na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki katika kanisa lao ambapo alipendelea sana kupiga Drums na gita.
KUHUSU FAMILIA YAKE
Familia anayotokea Barnaba ina jumla ya watoto watatu wakati Barnaba akiwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kutoka kwenye familia ya Mzee Barnabas.
MAISHA YAKE BINAFSI
Barnabas bado anaishi nyumbani kwao maeneo ya kigogo ambapo anaishi na familia yake.
Kila mwisho wa juma Barnabas huwa anapendelea kutembelea katika ufukwe wa bahari.
FALLY IPUPA ALIMSHAWISHI KUIMBA.
Barnabas alishawishiwa sana na msanii wa bolingo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) FallyIpupa , kuimba muziki kutokana na kuwa ni mwanamuziki pekee wa anayemvutia barani Afrika..
MBALI NA MUZIKI;
Mbali na muziki Barnabas anajihusisha pia na shughuli za biashara za uuzaji wa vyakula kwenye duka lake lililopo maeneo ya Kinondoni.
KWA MUDA GANI AMEKUWA AKIIMBA?
MIPANGO YA BAADAE YA BARNABAS KIMUZIKI
Mpango mkubwa na wa kwanza wa Barnabas ni kurudi shule, na hii ni kutokana na ukweli kuwa yeye hakuweza kubahatika kuendelea na masomo hadi ngazi ya juu ya kielimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: