Mkuu wa mkoa wa Rukwa Daniel Ole njoolay (pichani) amezitaka baadhi ya taasisi au vikundi kuanzisha bank ya wananchi katika Maeneo ya Inyonga ili kuwawezesha wakulima wa Kilimo cha Mpunga, karanga na Tumbaku kuhifadhi pesa zao mahara salama .

Mkuu huyo wa mkoa alizungumza hayo wakati akifanya tathmini ya ziara yake aliyoifanya Wilaya ya Mpanda na maagizo mbalimbali juu ya sekta hiyo.

Akizungumza na watendaji wa halmashauri mbili za Wilaya ya Mpanda na Mji Njoolay amesema kama banki hizo za jamii zitaanzishwa zitaepusha tatizo la kupolwa na kuhifadhi pesa hizo chini ya magodolo kama baadhi ya wakulima wanavyofanya sasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: