Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na WellShare International inadhamini mashindano ya mbio za riadha za nusu Marathoni zinazoitwa “Mbio za Ngorongoro” zitakazofanyika april 4 katika Wilaya ya Karatu. Mbio hizi zina lengo la kupiga vita ugonjwa wa Malaria.

Akiongea na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando (pichani) alisema kuwa Mbio hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya nne mfululizo chini ya udhamini wa Tigo, Mwaka huu mbio hizi zitakuwa kama sehemu ya utangulizi wa kuazimisha siku ya Malaria duniani itakayofanyika april 25 mwaka huu mkoani Arusha.

Alisema kuwa wanariadha mmoja mmoja na kama timu watajumuika na jamii ya watu wa Karatu kushiriki mbio hizo ambazo zitaanzia geti la Ngorongoro Crater na kuishia Karatu Mjini. Mwaka jana mbio hizi zilihudhuriwa na watu zaidi ya 5,000 ambapo wakazi wa wilaya ya Karatu walijifunza mambo mbalimbali yahusuyo magonjwa, zaidi ikiwa ni ugonjwa malaria.

Tigo imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano inayochangia shughuli za maendeleo ya afya na hivyo kuonyesha uzalendo uliyotukuka kwa kuwajali wananchi ambao ndiyo wadau wao wakubwa.

Wadhamini wengine ni Shirika La Maendeleo La Watu wa Marekani (USAID), Kampuni ya utalii ya ZARA, A to Z Textiles/Olyset Nets, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Halmashauri ya Wilaya ya Karatu. Halikadhalika wafanyabiashara mbalimbali wa Karatu wakiwemo Jubilee Tyres, Karatu Quality Garage, Bougainvillea Lodge na Octagon Lodge, Happy Days Pub, Karatu Bakery, Shagri-La Estates, pamoja Exim Bank.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: