Mke wa Mkemia Mkuu wa Serikali Marehemu Ernest Mashimba mama Rose Ernest akisaidiwa na ndugu wakati alipopita mbele ya jeneza la marehemu mume wake wakati wa kuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake jijini Dar es salaam, mwili wa Marehemu mashimba umesafirishwa jana kwenda kijiji cha Ngudu Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi. Marehemu Ernest Mashimba alifariki wiki iliyopita kwenye hoteli ya Executive Inn Lushoto mkoani Tanga alikokwenda kwenye mahafali ya mtoto wake Happy Ernest aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani humo.
Mtoto wa Marehemu aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari ya Kifungiro mkoani Tanga Happy Ernest Mashimba akiuaga mwili wa marehemu baba yake kwa majonzi makubwa. Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la bwana lihimidiwe, mungu aiweke roho ya marehemu Ernest Mashimba mahali pema peponi AMINA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: